Klabu ya Manchester City, wamefanikiwa kumng’oa Rodri staa kutoka Atletico Madrid! Nyota huyu anatimba kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kwa paundi milioni 70.
Rodri ananaingia kwenye orodha kama mchezaji aliyenunuliwa kwa dau kubwa zaidi. Wachezaji wengine ambao wamewahi kununuliwa kwa dau kubwa ni;
Riyad Mahrez alisajiliwa Julai 2018 kwa dau la paundi milioni 60. Dau lake lilikuwa ndiyo dau kubwa zaidi kuwahi kufikiwa na klabu hiyo katika usajili, na sasa paundi milioni 70 zilizomvuta Rodri zimezima rekodi yake.
Kevin De Bruyne alisajiliwa kwa paundi milioni 55 August 2015 na kukatisha rekodi iliyoandikwa na mtangulizi wake miezi mmoja tu uliopita. De Vruyne alitokea Wolfsburg.
Raheem Sterling alisajiliwa kwa paundi milioni 49 akitokea Liceverpool Julai 2015. Kwa wakati ule alikuwa kama mmoja wa wachezaji gharama zaidi kwenye historia ya soka la Uingereza. Rekodi yake iliishi kwa mda mfupi, mwezi mmoja tu baadaye rekodi yake ikavunjwa na Kevin De Bruyne.
Aymeric Laporte aliingia Man City kwa paundi milioni £57 akitokea Athletic Bilbao Januari 2018.
Hawa ni baadhi ya mastaa waliovunja vibubu kwa klabu ya Man City kwa nyakati zao.



Povel
Duh pesa ndo kila kitu
Furahav
Yuko safi