Frank Lampard, Meneja Mpya Chelsea

Klabu ya Chelsea imemteua aliyewahi kuwa kiungo wa klabu hiyo Frank Lampard kuwa meneja wao mpya. Frank Lampard anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Maurizo Sarri.

Lampard mwenye miaka 41, anaingia klabuni hapo akitokea Derby County, aliitumikia klabu ya Chelsea kwa miaka 13 akliwa kama mchezaji.
Lampard anakuja Chelsea akihitajika kujiandaa kukutana na changamoto juu ya namna ya kuwatumia wachezaji waliopo wakati klabu hiyo ikitumikia adhabu ya kufungiwa kufanya usajili.

Mkurugenzi wa klabu ya Chelsea, anasema imekuwa ni furaha kubwa kumkarisha nyota huyo aliyeitumikia klabu hiyo kwa mda mrefu kuwa kama meneja wa klabu. Anaamini Frank Lampard ni moja kati ya mameneja vijana wenye vipaji vikubwa kwenye soko la soka.

Alipokuwa mchezaji wa klabu hii alicheza Jumla ya mechi 648 kwa Chelsea, akishinda mataji 11 makubwa klabuni hapo. Ameeleza wazi kuwa mapenzi yake na Timu ndiyo yaliyompa historia inayoendelea dhidi ya klabu hiyo. Sasa anajipanga kukiandaa kkosi kwa ajili ya msimu ujao.

Acha ujumbe