Kila siku kunakuwa na mambo mageni, ya kufurahisha na yanakuwa na sura ya pekee kwenye soka. Frenkie de Jong aliwafurahisha sana wadau wa Ajax kipindi alipokuwepo klabuni hapo mpaka. Wadau wameamua kukodi basi kwenda kumshukuru Dejong.
Frenkie De Jong alikamilisha uhamisho wa kutoka klabuni hapo kwenda Barcelona mwezi Januari kwa dau la paundi milioni 75. Kutambua mchango wake mkubwa klabuni Ajax, staa huyu atakumbukwa klabuni hapo.
Basi lililokodiwa limepambwa picha ya mwanasoka huyu na kuandika kujumbe kwa Barcelona. Ujumbe unaotumwa kwa Barcelona unasomeka kwa kingereza “Barca, enjoy the future like we do” ukimaanisha kuwa klabu ya Barcelona nayo ifurahie kesho yake ikiwa na staa huyu kama wao.
Basi hili limepewa ratiba ya kuzunguka mji mzima ndani ya hispania kumtakia heri kinda huyu aliyecheza jumla ya gemu 89 za Ajax baada ya kujiunga na klabu hiyo mwaka 2015.Kwa
Issa
De jong fundi barca umepata mtu