Magoli 100 ya Haraka PL

Ligi Kuu ya Uingereza imeshuhudia wachezaji wengi wakiweka historia ya kutikisa nyavu mara 100 wakiwa katika umri mdogo kabisa. Kama ilivyo ada kufikisha idadi hiyo ya magoli ni ndoto ya kila mchezaji ambaye anacheza katika safu ya ushambuliaji ili kujikusanyia idadi kubwa ya magoli. Wafuatao ni baadhi ya wachezaji hao:

Michael Owen

Pamoja na mengine makubwa aliyoyafanya yenye mafanikio lakini ni Muingereza wa mwisho kabisa kupokea tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2001. Alifikisha idadi hiyo ya magoli alipokuwa na Liverpool. Alifunga idadi hiyo akiwa Anfield mara baada ya kucheza mechi 186 kwa wakati huo akiwa na miaka 23 na siku 133. Pia, alichezea klabu kama Real Madrid, Newcastle United, Manchester United na Stoke City.

Robbie Fowler

Mchezaji ambaye Liverpool hawawezi kabisa kumsahau kwa kile alichokifanya akiwa na klabu hiyo. Alithamini kucheza hata makosa ilmradi aisaidie timu ipate matokeo, alifikisha idadi hiyo akiwa na miaka 23 na siku 282 baada ya kucheza mechi 174 tu. Mbali na Liverpool aliweza kuchezea Manchester City na Leeds United.

Wayne Rooney

Mchezaji wa zamani wa Everton na Manchester United ambaye ni kati ya Waingereza waliojenga historia kubwa kwenye soka. Alifikisha magoli 100 akiwa na umri wa miaka 24 na siku 99. Pia, ameweza kuvunja rekodi ya Sir Bobby Charlton kufunga magoli mengi akiwa na miaka 40. Kwa sasa anamalizia historia akiwa MLS na DC United.

Harry Kane

Mfungaji hatari wa Tottenham ambaye amekuwa akiipa ushindi timu hiyo mara kwa mara. Aliweza kufikisha idadi hiyo katika msimu wa 2017/18 mbele ya Liverpool akiwa na miaka 24 na siku 191. Amefikisha idadi hiyo akiwa na jumla ya mechi 141 tu za ligi hiyo. Na kwa umri wake bado ana safari ndefu ya kuendelea kuchungulia nyavu na kuvunja historia zaidi akiwa na Spurs au hata akisajiliwa nje ya Spurs.

Romelu Lukaku

Mshambuliaji huyo wa Manchester United, aliweza kumshusha Alan Shearer kwenye nafasi hiyo ambaye alifikisha magoli 100 baada ya mechi zake 124 akiwa na umri wa miaka 25 na siku 137 pekee na kukaa katika nafasi ya tano. Katika mafanikio yake amekuwa ni mchezaji wa nje ya Uingereza kufikisha idadi hiyo ya magoli akiwa na umri wa miaka 24 na siku 322. Aliweza pia kuzichezea klabu za Everton na West Brom.

4 Komentara

    Yupo vizur sana

    Jibu

    Wako vizuri.

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Historia ya ukweli

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.