Staa wa Manchester United Paul Pogba amekuwa akihusishwa na kuihama klabu ya Manchester United, lakini haijafahamika mpaka sasa ni lini na klabu gani hasa anatarajia kuwepo.
Wakala wa mchezaji huyu ameweka wazi kuhusu nia ya staa huyu kuihama Man U na kusisitiza kuwa kila mtu anajua yale yanayomsibu Pogba katika mpango wake wa kuhama.
Pogba haioni kabisa kesho yake klabuni Manchester United na alinukuliwa akiviambia vyombo vya habari kuwa anahitaki kwenda kupata changamoto zingine mahali pengine.
Klabu zinazohusishwa zaidi na staa huyu ni klabu za Real Madrid na klabu ya Juventus. Zinedine zidane aliweka wazi kuvutiwa kwake na staa huyu baada ya Pogba kusema kuwa kuwepo Real Madrid ni ndoto kwake. Hata hivyo taarifa zinadai kuwa Real Madrid tayari wameshaamua kuachana na mpango wa Pogba kwa sasa, huku Juventus wakitajwa kuwa kwenye jitihad za kumrejesha nyota huyu klabuni hapo.
Pogba alikuwa anatarajiwa kuwepo kwenye maandalizi ya msimu ujao akiwa na Manchester United, lakini staa huyu hajakuwepo kwenye wiki ya mafunzo ya maandalizi ya msimu ujao.
Raniola anasema kila mtu anatambua utayari wa Paul Pogba kuondoka klabuni hapo. Staa huyu mwenye miaka 26 amekuwa akibeba lawama kutoka kwa baadhi ya wadau na mashabiki wa Man United licha ya jitihada zake alizoonesha msimu uliopita.
Mkataba wa sasa wa Pogba wa Manchester United unafika tamati mwaka 2021. Moja ya kikwazo cha staa huyu kuhama kwa sasa ni daula uhamisho na mshahara wake mkubwa ambao baadhi ya klabu zinahofia kuwa zitashindwa kumlipa.


Issa
Pogba