Alvaro Morata Kubaki Atletico Mazima

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata anatarajiwa kuungana na Atletico Madrid kwenye dili la kudumu baada ya kuitumika klabu hiyo kwa mkopo.

Mkataba wa Alvaro kuwepo Atletico kwa mkopo kwa miezi 18 unafika tamati mwisho wa msimu ujao, amekuwepo klabuni hapo tokea mwezi Januari.

Morata pia aliwahi kuchezea klabu za Real Madrid na Juventus, ameichezea klabu hiyo gemu 17 na kucheka na nyavu mara sita toka alipoingia klabuni hapo. Akiwa Chelsea alicheza Jumla ya mechi 72 na kufunga magoli 24.

Morata, mwenye maiaka 26, ambaye anafurahia kupata dili la kudumu klabuni hapo amechapisha kwenye kurasa zake kuwa anafuraha kufuatia tamko rasmi la klabu.

Tamko la Atletico Madrid linathibitisha, linasomeka;
“Mshambuliaji Mhispania ataichezea klabu yetu kwa kipindi cha mkopo, kama tulivyokubaliana alipokuja Atletico kwenye dirisha la mwezi Januari, na uhamisho wake utakuwa wa kudumu mwanzoni mwa semister ijayo.”

3 Komentara

    Morata ni mshambuliaji mzuri sana.

    Jibu

    Morata abaki tu

    Jibu

    Morata hapo ni pako tu madrid

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.