Kinara wa kucheka na nyavu klabuni Liverpool, Mohamed Salah anahofiwa kukosekana kwa hadi miezi 4 msimu ujao baada ya kubadilishwa kwa ratiba za michuano ya Olympics mwaka huu na pia kubanwa na ratiba ya Kombe la Mataifa ya Africa.
Nyota huyu ambaye kwa sasa ameshikilia idadi ya magoli 16 katika mechi 26 za Ligi Kuu ya Uingereza, amechangia kwa kiasi kikubwa kuwaweka Liverpool katika nafasi waliyopo sasa wakiwa na rekodi ya pointi 25 zaidi ya wapinzani wao.
Mabadiliko ya michuano ya Olympics ambayo ilipangwa kufanyika mapema Julai 24 hadi Agosti 9 mwaka yatakuwa kikwazo kwa Salah kutekeleza majukumu yake katika klabu ya Liverpool. Michuano hii ambayo sasa imepangwa kufanyika mwaka 2021 yanatarajiwa pamoja na Michuano ya Kombe la Africa kuingilia ratiba za EPL. Hii itamlazimu Mo Salah kukosekana kwenye klabu ya Liverpool nyakati hizo kwakuwa anategemewa kuiwakilisha nchi yake katika michuano hiyo.
Meneja Jurgen Klopp mara kadhaa alilalamikia uamuzi wa mabadiliko ya michuano ya kombe la mataifa Africa na kusema kwa upande wao hilo ni kama janga. Hivyo ikiwa ratiba hazitakuwa rafiki na EPL, Liverpool watamkosa Salah kwa miezi karibia minne.


Janeflora malisa
Ni mchzj mzr na itawaconst sana clabu yak maan ni mchzj tegemez