Tony Ferguson atapambana na Justin Gaethje katika UFC 249

Justin Gaethje amechukua rasmi nafasi ya Khabib Nurmagomedov katika pambano la #UFC249 na atakutana na Tony Ferguson kwenye pigano la uzito wa kati. Ferguson alitakiwa Aprili 18 kukabiliana na Mrusi Khabib ambaye hajawahi kupoteza pambano lolote kwenye UFC, lakini kutokana na janga la sasa la Covid-19 Khabib alitangaza kutoshiriki pambano.

Rais wa UFC Dana White amethibitisha kwamba Gaethje, kama inavyotarajiwa, atachukua nafasi ya Khabib, na atakabiliana na Ferguson kwenye UFC249 uzani wa kati.

Dana White

Tony anaetambulika kwa jina la utani la El Cucuy lenye maana ya Mzimu ilitakiwa pambano lake linalo fuata apambane na mrusi Khabib Nurmagomedov mwezi Aprili katika maeneo ya Brooklyn jijini NewYork nchini Marekani, ila pambano hilo lili ahirishwa kutokana na sharia za jiji la New York za kuzuia mikusaninyiko ili kujikinga na Janga la Korona.

Janga la korona limepekea Nurmegomedov kukimbilia nchini kwao Urusi na kujikuta hawezi kurudi Marekani kutokana na vizuizi vya kuto kuingia Marekani kwasababu ya janga la Korona. Na kusababisha Raisi wa UFC Dana White kuhamhamishia mshindani namba nne Justine Haethje  kuziba nafasi iliyo achwa na Khabib ili kuziba pengo hilo.

Justin Gaethje na Tony Ferguson

Kwa umaarufu wa jina la utani alilopewa la “THE HIGHLIGHT” kwa stile zake za kuonesha hasira na ubunifu wa kupambana ulingoni, Mshindi huyo wa NCAA aliejiweka kwenye vichwa vya habari kwa kupiga wapinzani wake kwa K.O ndani ya dakika ya kwanza kwa mapambano matatu mfululizo.

Gaethje aliripotiwa kupambana na Connor McGregor kwenye wiki ya  mapambano ya kimataifa  ya mwezi Julai.

 

2 Komentara

    Mmh hili pambano noma sana.

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.