Klabu ya Manchester United inatajwa kuwa na mazungumzo na Jorge Mendes kuhusu uwezekano wa kufanya biashara na klabu ya Real Marid. United wanatajwa kuwa wanamtaka kiungo Mshambuliaji James Rodriguez.
Staa huyu ambaye alishinda Kiatu cha Dhahabu kwenye Kombe la Funia la mwaka 2014, anaonekana yupo tayari kuondoka Bernabeu mwisho wa msimu baada ya kuwa na msimu mgumu kiasi chake klabuni hapo. Amecheza gemu 13 tu msimu huu kufuatia shida ya majeraha na kutokuwa kwenye fomu nzuri.

Real Madrid watakuwa na nafasi ya mwisho kumuingiza sokoni staa huyu katika msimu wa usajili unaofuata kwa kuwa mkataba wake unafiika tamati msimu ujao.

Kwa mujibu wa chapisho la AS, maofisa wa Old Trafford tayari wameshafanya mazungumzo na wakala Mendez kufuatia uwezekano wa kukamilisha biashara hiyo.
Tetesi zinasema kuna uwezekano Paul Pogba akahusika katika mabadilishano kipindi hiki akiwa anashinikiza nia yake ya kutaka kusepa United. Pogba aliwahi kuweka wazi kuwa anapenda kuwepo Real Madrid, dili hili likifanyika utakuwa ni wakati wake kupeta Madrid.

