Soka Tamu Ila Ubaguzi Unaharibu!

Kuna kipindi soka la Ulaya linakuwa tamu la kuvutia linalopendwa kuonekana mbele ya shabiki yeyote yule duniani. Kiujumla wachezaji wanajituma, akili na miili yao yote inafanya kazi moja tu: kuhakikisha timu inapata matokeo. Ila kuna kipindi mtu au kikundi cha watu wasio na utu, akili au wivu pengine kwa makusudi au kwa bahati mbaya wanaamua tu kuleta ubaguzi ili kuwatoa wachezaji mchezoni. Hiki kitendo cha rangi nyeupe kujiona wao bora kuliko wale wengine weusi inakera na kuondoa kabisa morali ya kazi. Tuseme tu ni wivu au jazba za mchezo maana kuna baadhi ya wachezaji walijikuta wanatumbukia kwenye ufedhuli huo wa kubagua wenzao mchezoni hasa kwa lugha au ishara zisizofaa.

Ubaguzi

Wachezaji kama Milan Baros, Sergio Busquets, John Terry na Peter Schmeichel ni miongoni mwa wachezaji waliowahi kutumia lugha hizo zisizofaa kwenye michezo.  Huku wachezaji wengi wenye walau kidogo tu uweusi wamekumbwa na kebehi hizo, wakina Marcelo, Ashley Cole, Ashley Young, Boateng, Daniel Alves, Neymar hadi Sala huku Waafrika wengi wakikumbwa na lugha hizo za kibaguzi. Wabaguzi hawakuishia hapo bali wanakebehi hadi timu za taifa ikiwemo ile ya Senegali ilivyokebehiwa kule Asia, Zambia na South Afrika. Ingawaje ubaguzi haupo Ulaya tu kwani Asia, Marekani upo ila Ulaya katika soka wao ni magwiji ligi zao ni bora na wanatunga sheria nyingi kandamizi kupunguza au kuzuia kabisa hali hiyo ya ubaguzi wa rangi ila wapi!

Kumekuwa na hukumu mbalimbali ikiwemo kutoa faini, kufungiwa mchezaji husika asicheze au kushiriki michezo kadhaa. Mfano, Milan Baros akiwa Olympique Lyon alimtolea kitendo vya kibaguzi Mcameroon, Stephen M’bia kwa kumbania pua na kumfanyia mikono kuwa ampishe, kitendo hicho kilitafsiriwa ni ubaguzi chenye maana kuwa M’bia ananuka na asimguse Baros. Japokuwa Baros alijitetea kuwa alimwambia M’bia kuwa, “…nipishe, nipe nafasi ya kupumua” ila alipata adhabu ya kufungiwa mechi tatu. Urusi na Uhispania vilitozwa faini ya paundi 40335 wote kwa pamoja kutokana na vitendo vya kibaguzi mwaka 2012 kutoka na mashabiki wao kuimba nyimbo za kibaguzi. Romania na Ugiriki walipewa adhabu ya kucheza bila mashabiki mwaka 2018 kila mmoja kwa wakati wake tofauti.

FIFA

UEFA pia wakaanzisha kampeni mbalimbali ikiwemo ile ya, “…say no to racism” wakimaanisha sema hapana kwa ubaguzi wa rangi. Pia, ile ya “…say no to racism – my game is fair play” ikimaanisha kupinga ubaguzi wa rangi – na mchezo wangu ni wa kiungwana, iliyoanzishwa na FIFA, shirikisho la mpira duniani kisha wachezaji wa timu zote hupiga picha wakichanganyika pamoja na waamuzi wa mchezo huo. Hiyo yote ni kuhakikisha usawa katika mchezo pia kucheza pasi na kujali rangi, umbile wala mahali alipozaliwa mtu.

Wachezaji wamekuwa na mapokezi tofauti pindi wanapofanyiwa vitendo vya kibaguzi. Boateng yeye aliamua kutoka nje ya uwanja baada ya kufanyiwa vitendo vya kibaguzi mwaka 2013 akiwa anachezea klabu ya AC Milan wakicheza dhidi ya Club Pro Patria ya huko huko Italia pia Mousa Marega wa Porto naye alifanya hivyo hivyo mwaka huu. Romelu Lukaku yeye alijizuia na baada ya kuandika kwenye mitandao kuwa aliwaona waliokuwa wanamzomea kama machizi tu. Mario Balotelli yeye aliandika maneno haya, “…small mind and imbecile” akimaanisha kuwa wana ubongo mdogo na ni wapumbavu.

Ajabu ni kuwa Daniel Alves yeye alienda tofauti kabisa na wenzake. Yeye alitumia ule usemi wa kutumia mawe wanayakutupia maadui kama ngazi ya kuwafikia walipo. Yeye alipotupiwa ndizi na mashabiki wa Virrareal alichukua ndizi hiyo akaimenya na kuila na akapata motisha ya kuipa timu ushindi, ndiyo kwani kwenye mechi hiyo Barcelona walishinda 3-2. Kikubwa ni kuwa kila mtu ana namna yake ya upokeaji wa taarifa, kuna wanaohamaki na kuchukia na wapo wanaochukulia simple tu yaani kawaida. Ila yote kwa yote kubaguliwa kunakera na kunaumiza itabidi FIFA watoe adhabu kali zaidi walau kupunguza suala hili.

3 Komentara

    Duuh ni bora waache ubaguzi maana sio mzuri

    Jibu

    Ubaguzi sio jambo zuri Ila sheria inatakiwa ifuatwe na pia itende haki katika swala la ubaguzi

    Jibu

    Ubaguzi wa rangi sio mzuri kabisah inabidi sheria ifate mkondo wake kea sababu hii inaweza kupelekea hata kwa mchezaji kuwa kwny kiwango tofauti sna

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.