Laila Mohamed Ali Alivyodhirisha Vya Kurithi Vinazidi!

 

Kwa mara ya kwanza alipomtaarifu baba yake kuwa anataka kuwa mwanamasumbwi kama alivyokuwa yeye, Mohamed Ali, bingwa namba moja katika historia ya mchezo huo duniani alipatwa na fadhaa. Hakuwa na jibu la moja kwa moja kuwa sitaki wala ndiyo, kilichompa mawazo kidogo ni kuwa inakuaje mtoto wake wa kike ndiyo atamani kuwa kama yeye? Ingawaje Ali alikuwa na watoto wa kike wengi ila pia alikuwa na wa kiume wawili. Ali alikuwa na watoto 9 lakini kati ya watoto wake wote mtoto wake mmoja tu ndiyo alitamani kuwa kama yeye. Kimsingi Laila alishafanya maamuzi hayo magumu ya kuwa bondia hivyo alitaka baraka tu kutoka kwa baba yake. Ijapokuwa Muhamed Ali alijua fika uchungu wa ngumi ila mwishowe alikubali yaishe, tuseme tu alisema ule msemo wa Kiswahili, “…mtoto akililia wembe mpe”. Eeeh ukimkata ndiyo atajua madhara yake.

Laila aliyezaliwa Desemba 30, 1977 huko Miami Beach Frolida nchini Marekani, ni mtoto wa nane na wa mwisho miongoni mwa aliowazaa mwenyewe, kimaana huyo wa tisa alimkuta kwa mkewe wa nne. Mohamed Ali ambaye alizaa na mke wake wa tatu aitwaye Veronica Porche Ali ndiyo akampatia binti huyo Laila. Alisoma na kamaliza chuo cha California Santa Monica College huko Marekani huku akipata shahada ya biashara akiwa na miaka 16 tu. Alipomaliza chuo akajihusisha na mambo ya urembo, si unajua wanawake kwa urembo hivyo Laila alikuwa na saluni yake ya urembo wa kucha huko huko Marekani. Ingawaje baba yake alikuwa mpambanaji nguli ila Laila hakuingia kwenye masumbwi kutokana na kushawishiwa na baba yake bali pale alipoona mapambano ya wanawake kwenye runinga ndiyo akavutiwa na mchezo huo.

Laila aliamua kujihusisha na masumbwi pale alipofikisha umri wa miaka 18. Na kwa kuwa alikuwa maarufu kutokana na kazi ya baba yake hivyo ikawa ni rahisi kwake kujitangaza kuwa ana nia ya kuwa bondia wa kimataifa. Katika kipindi cha Good Morning Amerika Laila alihojiwa na mtangazaji Diane Sawyer na kuelezea dhamira yake hiyo. Mwanzoni ilikuwa vigumu kwa Mohamed Ali kumkubalia mwanawe kujihusisha na mchezo huo lakini kutokana na ushawishi na nia aliyoiona kwa mwanawe ikabidi tu akubali kishingo upande. Tuseme tu Mohamed Ali hakutilia maanani upambanaji wa masumbwi kwa wanawake.

Laila Ali alianza kupambana mwaka 1999 Oktoba 8 na mpambanaji April Fowler katika ukumbi wa Turning Stone Resort & Casino huko Indian Nation, Marekani. Ingawaje lilikuwa pambano lake la kwanza ila waandishi wa habari pamoja na mashabiki wa masumbwi walijaza uwanja ili kumshuhudia binti wa nguli Mohamed Ali. Kila mtu alitaka kujua kuwa je, mtoto wa nyoka ni nyoka au laah! Na kweli Laila hakumuungusha baba yake, kwani alitumia sekunde 31 tu kumuangusha April, ilikuwa ni furaha iliyoje kwa mashabiki wa masumbwi kumuona binti wa Ali akifanya mambo aliyoyafanya baba yake. Baada ya mchezo huo Ali alimfuata mwanawe kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kumwambia, “…girl you bad” akimaanisha kuwa mwanawe ni mtu mbaya ila ni ya kumsifia kuwa shughuli aliyoifanya uwanjani si ya kitoto. Huo ukawa mwanzo mzuri wa Laila.

Kimsingi Laila alishafanya maamuzi hayo magumu ya kuwa bondia hivyo alitaka baraka tu kutoka kwa baba yake. Ijapokuwa Muhamed Ali alijua fika uchungu wa ngumi ila mwishowe alikubali yaishe, tuseme tu alisema ule msemo wa Kiswahili, "…mtoto akililia wembe mpe". Eeeh ukimkata ndiyo atajua madhara yake.Kisha akapata pambano jingine na kushinda zikiwa zimebaki sekunde tatu tu dhidi ya Shadina Pennybaker, kisha akashinda mengine tisa mfululizo. Kuanzia hapo watu wakatamani Laila apambane na watoto wa mwanamasumbwi wa zamani, George Foreman (Freeda Foreman) au Joe Frazier (Jacque Frazier Lyde). Na hatimaye June 8, 2001 Laila na  Frazier wakakutana. Waandishi wakaliita Ali & Frazier 4 wakimaanisha kuwa ni muendelezo wa mapambano kati ya George Foreman na Muhamad Ali. Ama kweli hakika mpambano huu wa mizunguko 8 ulikuwa mkali haswa, ingawaje Laila alishinda kwa maamuzi ya majaji ila alimaliza pambano akiwa anachuruzika damu puani na huku Jacque akiwa anachuruzika damu kwenye macho.

Laila alichukua mkanda wake wa kwanza wa (IBA) Agosti 2002 baada ya kushinda mzunguko wa pili dhidi ya Suzette Taylor. Kisha akaongeza mingine miwili mwezi Novemba mwaka huo huo, ule wa WIBA na IWBF baada ya kumtandika Valarie Mahfood kwa TKO kwenye mpambano wa mizunguko nane. Na baadaye kuutetea mkanda wake dhidi ya Mahfood mwaka 2003. Mwaka 2004, Laila akaongeza tena mkanda mwingine ila huu ukiwa wa uzito mwepesi wa juu, IWBF baada ya kumtandika Gwendolyn O’neil. Juni 2005 Laila alishinda taji la dunia kwa wanawake, World Boxing Council kwa kumpiga Erin Toughill hivyo kuwa mwanamke wa pili baada ya Jack Nava. Ikumbukwe kuwa Laila alipigana katika uzito wa kati na ule wa juu mwepesi tofauti na baba aliyepigana uzito wa juu.

Februari 2 mwaka 2007 Laila Ali alimpiga tena Gwendolyn O’neil katika raundi ya kwanza tu kwa TKO na huo ukawa mpambano wa mwisho kwa Ali. Kiujumla alicheza mapambano 24 na kushinda yote 21 akishinda kwa KO huku matatu akishinda kwa maamuzi ya majaji. Hapo ndipo ule usemi wa vya kurithi vinazidi kwani Mohamed Ali pamoja na ubora wake wote ule lakini alichezea kichapo ila mwanawe Laila Ali hakuruhusu kupigwa katika historia yake ya masumbwi.

Kimsingi Laila alishafanya maamuzi hayo magumu ya kuwa bondia hivyo alitaka baraka tu kutoka kwa baba yake. Ijapokuwa Muhamed Ali alijua fika uchungu wa ngumi ila mwishowe alikubali yaishe, tuseme tu alisema ule msemo wa Kiswahili, "…mtoto akililia wembe mpe". Eeeh ukimkata ndiyo atajua madhara yake.

Nje ya masumbwi Laila ameolewa na Curtis Conway na wamejaliwa watoto wawili. Pia, amejitokeza mara nyingi kwenye vipindi vya televisheni ingawaje Mohamed Ali alikuwa Muislamu ila Laila hakufuata kabisa imani ya baba yake. Uzuri ni kuwa ubabe wa baba ukahamia kwa mtoto ingawa naye alishastaafu ila tulipata burudani kutoka kwao wote wawili.

2 Komentara

    Sawa kabisa maji hufuata mkondo

    Jibu

    Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.