Juventus wanaripotiwa kuwa wamemuongezea likizo nyota Gonzalo Higuain kwa sababu binafsi. Taarifa zinaonya kuwa hii inawezekana kuwa ni hatua katika mpango wa kuondoka klabuni hapo.
Kwa mujibu wa chapisho la Tuttorsport, staa huyu ameongezewa mda wa siku tano zaidi wa kurejea klabuni hapo. Higuain anatarajiwa kurejea kutoka Argentina baada ya kuisha kwa mda alioongezewa.
Taarifa zinataja kuwa staa huyu amekawia kurejea Italia kwa sababu aliamua kuwa na mama yake ambaye anagua, na hakuwa anapenda kumuacha mama yake huyo peke yake. Huenda hii ikawa ni hatua moja kuelekea mpango wake wa kuondoka klabuni hapo.
Wachezaji wengine ambao waliamua kuondoka Italia, baada wakati kukiwa na masharti ya kusalia karantini tayari wamerejea. Juventus bado inamkosa pia Adrien Rabiot.
Wachezaji wote wanaorejea Italia wanatakiwa kukaa karantini kwa lazima kwa angalau wiki 2. Klabu bado hazijaanza mazoezi ya makundi kama timu, hivyo bado wachezaji wanaweza kufanya mazoezi wakiwa popote.
Ripoti zinasema Higuain, pamoja na mwenzake Rabiot wameiweka klabu katika sintofahamu kwakuwa hawakutarajiwa kama kufanya hivyo, hivyo suala hili linatarajiwa kuathiri hatma ya wachezaji hawa pale Juventus.


Rehema Dickson
Popote kambi mazali kipaji anacho vizuri tu
aisha
kwakua anakipaji hainashida
Ester mmakasa
Akufukuzae hakwambii toka, hii si sawa kabisa maana fundi kama higuain huwezi kumpa likizo kama hizo.
felister
co vzr kumuongezea likizo km hajaiomb labda km aliomba aongezewe
Hamidu
Tatizo umri.lkn bado ni mchezaji nzuri.
Ila kwa timu ndogo hatawasaidia
Emnmy cleopa
Anakipaji kinzur sana anaweza hata akawasaidia timu ndogo ndogo
Dorophina
Anakipaji atasaidia maana timu ni bado kiuwezo
Rehema
Duuuhhh hii Kali, kunani??!!
amon
kawaida kwa mchezaji kutoka tmu moja kwenda nyngne ilo ndio chaguo lake
Magdalena
Duhhhh
silva tira
huku kazi huku familia
mathayo sonje
kama manager hamtaki mchezaji ni bora kumuuza kuliko kumpa likizo zisizo na sababu, haiwezekani HIGUEIN kusugulishwa benchi na ubora alionao
Agness
Yuko vizuri popote anafaa
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo vizuri anajua kokote kambi
Antony Luseno
Endapo kama hajaridhia mwenyewe sio poa
Frank patrick
Jamaa ni straiker mzuri ila umri nao Ndio hata kwenye maswala binafsi unamfanya wamuhishanishe na kuhamishwaa
Kenani
Sas likizo anabewa kakupenda ama ya lazima
Isaya massawe
Ataenda Madrid bado ana kiwango kizur
Furahav
Ataenda yanga huyo.
David Pere
Maisha yapo sehemu yoyote ile ,kinatakiwa kiwango kiwe juu tu
Lombo
mmmh akufukuzae akwmbiii tooooka
Shafii
Uwezo kwa higuian umeisha na umr unamtupa mkono
Mariam
Duuuh
Samiah
Kambi popote
Tahiya
Bdo ni mchezaji mzur pamoja na kuwa umri Umesogea
Salma
Bado yupo vizuri
Ernest Kimeru
What is goin on with Higuain?
Theckla
Kuonewa kwake ndo kutengenezewa njia hivyo asife moyo
nasra
Bado anauwezo mzuri
SADICK
Kuuguza ni jambo kubwa hivyo alisitahili kuongezwa siku za likizo
Neema hassan
Popote kambi ila anapoenda lazima kuwe na maslahi..
Mwajuma
Siyo vibaya Kumpa likizo
Ester jackson
Kazi na umri apumzike
geniaskaluzwe8
Duuuuh
Neema juma
Ila kipaji cha mtu hakipoteii asiwe na wasiwasi japo waswahili wanasema akufukuzaye hakuambii toka
winfrida
anaweza kurudi kwenye club yake kuongezewa likizo sio sababau
christopher
Huyu jamaa mpira umeshamshinda tayari cha msingi aende tu MLS au China akatafute pesa ligi za kiushindani pale ulaya haziwezi tena
Lombo
duuh akufukuzae akwmbiii tok
Mwanahamisi
Bado yupo vizuri
Asia Abdy
Duh sio poa
David pere
Kwahiyo kupewa likizo na kapata uhamisho kweli noma
Tatu
Ni vizuri kukaa likizo ili apumzike
Elika
Kipaji anacho
Swai
Nini kinaendelea??