Staa wa tenisi wa Marekani, Serena Williams anasema kwamba kwa sasa yupo tayari kucheza mchezo halisi wa tenisi baada ya kuwekwa karantini kwa muda sasa.
“Ninatamani sana kurudi uwanjani kucheza mchezo niupendao,” alisema mshindi huyo mara 23 wa Grand Slam wakati akiwasiliana na dada yake, Venus wakati wa mawasiliano yao walipokuwa wakifanya mazoezi kwa njia ya mtandao wa Instagram siku ya Jumanne.
“Ninaiweza sana. Ninapenda sana kuifanya!”
Tenisi na michezo mingine yote imeahirishwa mpaka ifikapo katikati ya mwezi Julai kutokana na janga la COVID-19 huku michuano ya French Open nayo ikiahirishwa mpaka majira yajayo wakati pia michuano ya Wimbledon nayo ikifutwa kwa mara ya kwanza tangu itokee vita ya dunia ya pili.
Serena anasema kuwa anaona likizo hii kuwa ni jinamizi la lazima.
“Naona kama mwili wangu ulihitaji kitu hiki kwa hakika ingawa sikuitaka kabisa,” alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye mara ya mwisho alishinda taji la Grand Slam mwaka 2017 kwenye michuano ya tenisi ya Australian Open. “Na kwa sasa ninajisikia vizuri kabisa. Ninajiona nimepumzisha mwili kiasi cha kutosha, nina afya bora sasa. Kwa sasa ninaweza kwenda nje kucheza michezo halisi kabisa.”
Dada yake mkubwa, Venus, mshindi mara saba wa tuzo ya Grand Slam, alianza kuposti mazoezi yake kupitia mtandao wa Instagram wiki nane zilizopita ambapo akamualika mwenzake wiki hii, dada yake huyo wanapatana sana na akamkaribisha katika mazoezi aina ya yoga ikiwa ni sehemu ya kusogeza muda ili kungoja kurudi kwa michuano yao.
Serena alisema kwamba mazoezi, ambayo yanawachukua muda wa saa moja na nusu, ilikuwa kama changamsha mwili kwake, ingawa hawakuwa vyema sana kimwili wakati huo.
“Usijiumize mwenyewe wakati ukifanya hilo.” Alifunguka wakati gulani na akamshauri mwenzake. “Endapo ukiwa na magoti mabaya kama yangu hakikisha unatumia pad kucheza.”


Theckla
Serena anajua Sana tenes na asichoke kufanya mazoezi na kufata ushauri unaotolewa dhidi ya hili janga la corona muda utafika Mambo yatakaa shwari na aterejea tu uwanjani
mwakalosi
Wafanye wepesi tenesi
Irudi serena mwili unamuwasha
Ester mmakasa
Ni mchezo mzuri sana ila mm siuelewagi hata nikijitahidi kuufwatilia.
frank patrick
Moja kati ya michezo ninayoenjoy kuitazama kwa sasa
lombo
kama hali inaruhusu kaz ianze jamn tumemmis serena
Dorophina
Wafanye tenesi irudi wacheze tu ivyo ivyo bila mashabiki
winfrida
namkubali sana serena williams
Rehema
Wafanye tenesi inausika wacheze tu
Ernest
Ni swala la Kumuomba Mungu afanye wepesi juu ya Janga hili la Corona.
Povel
Serena anajuwaha sana tuweh na subir janga la coroa lipite
Aziza mushi
Serena anajua Sana namkubali.
Neema hassan
Serena William Yuko vizuri..
Carolyne
Mungu tuondolee janga la corona
Salma
Asante kwa taharifa
Asha
Asante kwa habar za kimichezo
Hope mwaikuka
Mungu atatenda na hal utarud kama zaman
felister
katika michezo siielewagi ni tenisi yani ata sijui goli linafungwa vipi
Asia Abdy
Serena hatar
Rehema Dickson
Serena mwenye meenyewe uyo
Ester jackson
Serena arudi jamani tumemiss
Gabriel
Sema Serena alishuka sana kiwango but matumain yapo Kama ameamua
Antony Luseno
Naona Serena ana gadhabu anataka aonyeshe makali yake
Emmy cleopa
Serena yupo vizur sana #meridianbettz
aisha
Serena ni mkali wa tenes
Genia Sikaluzwe
Serena yupo viziri kwenye tenes
Issa
Serena akijitahid miaka 5 ijayo atakua bado kweny ubora