Ni wakati mgumu sana ambapo wachezaji wameweza kujiuliza hatma zao katika michezo yao wanayoshiriki. Mmojawapo ni Bwana Lewis Hamilton ambapo mshindi huyo mara sita wa ubingwa wa dunia siku ya Jumapili alikiri kuwa amewaza sana juu ya hatma yake ya michuano ya Formula 1 wakati huu ambapo dunia imekumbwa na janga la Corona.
Amekuwa akihangaika sana kurudi katika hali ya ushindani kimchezo. “Kuna siku ninaamka nikiwa mwenye mawazo sana. Sioni haja ya kuendelea na mchezo wangu huu, tunaenda wapi? Nini kitafuatia? Niendelee kuendesha magari na kushiriki mbio za magari?”
Hayo ni maswali ambayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akijiuliza mara kwa mara. “Ninawaza juu ya haya mambo mengi sana, na kuishia kusema acha liwalo likawe tu. Na saa moja linalofuatia likiisha, ninasema tena, acha iwe. Ninapenda ninachokifanya. Na siwezi kusimama kushiriki mbio za magari.”
Msimu huu Hamilton anategemea kuifikia rekodi ya mwenzake Michael Schumacher aliyetwaa mataji saba ya dunia.
Hata hivyo, amekuwa hajui nini kitajiri kutokana na kusambaa kwa ugonjwa wa Coronavirus. Kutokana na jambo hilo mbio 10 zimesimamishwa na kuahirishwa kuendelea kwake.
Msimu mpya hautaanza mpaka pale ikifika tarehe 5 Julai nchini Austria endapo itawahi sana kuanza.
“Ni suala la kujiweka sawa kiakili. Ni namna ya kuangalia unajipenda zaidi wewe mwenyewe,” aliongezea Hamilton akiongea wakati wa Mental Health Awareness Week.
“Unatakiwa kujipenda zaidi na kuwa huru kwako mwenyewe.” Aliongezea: “Endapo hatujifunzi kitu wakati huu wa matatizo basi tujiulize ni nini tunachokifanya? Tunakuwa tunapoteza muda tukikaa bila ya kufanya kitu.”
Unadhani Hamilton ataikacha langalanga?


mwakalosi
ni muda wa kuishi nao huu ugonjwa maana sio ugonjwa wa kwanza kuna Spanish flu iliuwa watu wengi sana
Mwanaidi
Ni kweli lazima ajiulize maswali mengi ila sio yeye tuu ni watu wengi sana wamejiuliza sababu imewafanya warudi nyuma na kuyumba sababu ya huu ugonjwa hatatishi ila hizi ni changamoto kama chanagamoto nyengine kwenye michezo na mambo mengine ni suala la kumuomba sana mungu aepushie mbali na hali irudi kama zamani
Elika
Ugonjwa wa corona umeharibu mipango mingi sana lakini haina budi kuishi nao maana kuna mda tutasahau majanga na matatizo yote tuliopitia
Tahiya
Kwer nimaswali magumu na majibu yke ni fumbo kubwa mana hakuna anayejua huu ugonjwa utadumu kwa muda gani
Neema hassan
Hiki ni kipindi cha mpito kikubwa kuomba mungu huu ugonjwa wa corona uishe..
Rehema Dickson
Maswal lazima yawe mengi coz janga hili la corona lebadilisha mambo mengi sana michezo imesimama na ndo ajila,, familia inamtegemea na mambo mengine mengi ila mungu atafanya wepesi kila kitu kitakua sawa tu
Mariam mtandama
Duuuh
winfrida
usikate tamaa lewis ni mambo ya mapito kila kiyu kitakaa sawa na utarudi mchezoni
Evaluziga
Hiki ni kipindi kigumu Sana kwa ajili ya huu ugonjwa wa corona Cha msingi kuomba mungu atuepushe
Ester jackson
Endapo hawatajifunzi kitu wakati huu wa matatizo basi wajiulize ni nini wanachokifanya? Tunakuwa tunapoteza muda tukikaa bila ya kufanya kitu.”
Juliana
Mmmmh! Jamani don’t give up Lewis
Warda
Jamani Hamilton anapenda sana kazi yake #Meridianbettz
Hope mwaikuka
To be honest huu ugonjwa umeharibu kila ktu kwenye taratibu zetu
Aziza mushi
Maswali lazima yawe mengi sababu janga hili la Corona michezo imesimama Yani Ila mungu atafanya wepesii Mambo yatakaa sawa.
David pere
Huyu jamaa atatetea nafasi yake maana hakuna wa kushindana naye akiwa kwenye mashindano
Asha
Hamilton Lewis bonge la dereva kwny mbio za magar
Ernest
Hamilton ni tishio kwa sasa ulimwenguni
Frank Patrick
Aikache tu akapate challange nyingine na uongozi mwingine
Gabriel
Hawezi kuikacha langalanga na kuhusu covid 19 n jangw lisiloisha hvyo inabid tuishi nalo na mambo mengne yaendelee
Shafii
Hamilton yuko vizuri sana namkubali huyu jamaa
Emmy cleopa
Duuuh!! Ila usikate tamaa lewis
Povel
Duh asikate tamaaa aombe mungu tu
Asia Abdy
Hatar sana aisee
Caroline
Sema huo Mchezo ni atari
Magdalena
Ili gonjwa limetibua kila kitu Ila tu tuishi nalo kwa tahadhali
Zeiyana
Lazima tupate of huu uhonjwa unatisha sana kikubwa zaidi hauna kinga..!ni mwenyew tu kua makini lakini hauwezi kuukwepa na itachukua mda sana kuusahau
Amani
Ni suala la kujiweka sawa kiakili. Ni namna ya kuangalia unajipenda zaidi wewe mwenyewe
Theonestina
Daaah ili gonjwa lipite tu kwakwer
Kenani
Ugonjwa huu unawatia hofu watu wengi
Ester mmakasa
Mungu atusaidie huu ugonjwa uishe dunian maana bado tunaogopa sana.
Genia Sikaluzwe
Daaaah hatari corona siyo poa