Alphonso Davies – Pembeni yangu hapa nimetoka kukifunga kitabu cha Juddy Donnely. Kinaizungumzia safari ya binadamu watatu wa kwanza kwenda mwezini. Haikuwa safari nyepesi. Walitumia zaidi ya miaka 20 kuiandaa. Wakatumia miaka tisa kuishawishi serikali ya Marekani kuwapatia kibali. Baada ya mapigano mengi, hatimae waliruhusiwa na waling’oa nanga July 20 1969.
Haikutegemewa kuwa watarudi hai. Ila baada ya siku nne walitua salama pale Kaskazini mwa bahari ya Pacific. Mpaka leo majina yao wale binadamu yamesimama kwenye kuta za majengo ya NASA pale Washington DC. Neil Armstrong, Edwin Aldrin na Michael Collins. Nawaweka kando hapo kisha naufungua ukurasa wa Alphonso Davies.
Wazazi wa Alphonso Davies walikimbia Liberia kuokoa maisha yao
Wazazi wake waliikimbia Liberia baada ya vita kupamba moto mwaka 1999. Hawakuwa tayari kushika bunduki kwa ajili ya kutetea maisha yao. Hawakutaka kuendelea kupishana na maiti barabarani. Hawakutaka kuendelea kusikia sauti ya mabomu. Wakaamua kuondoka na kuishia Ghana Magharibi katika kambi ya wakimbizi. Huko ndipo walipompata Alphonso mwezi November mwaka 2000.

Baadae walipata mfadhili wa kuwatoa katika kambi ya wakimbizi, wakaondoka kwenda Canada Alphonso akiwa na miaka 5. Huko ndipo alipoanza maisha. Kwa kuwa wazazi wake hawakuwa na hela ya kumpeleka katika academy ya soka, alilazimika kuchezea timu ya kuwalea watoto wa mtaani kila jioni alipotoka shule. Soka lake likaanzia hapo.
Hapo ndipo alipoonekana na Vancouver Whitecaps, wakamchukua na kumpeleka katika academy yao. Baadae akapanda timu ya wakubwa. Bayern wakafanikiwa kumsajili July 2018 baada ya rais wa Barcelona kugoma kumsajili kwa kigezo kwamba hatokei taifa lenye historia ya soka. Ndiyo huyu Alphonso Davies tunayemuona leo kule kushoto kwa Bayern Munich.

Safari ngumu namna gani. Kutoka kupanga foleni ya chakula katika kambi ya wakimbizi hadi kuwa mchezaji bora chipukizi wa Bundesliga. Kutoka kucheza mitaani Canada hadi kupigwa buti na Lionel Messi. Safari ambayo kimawazo isingewezekana kufanikiwa kama ile ya kwenda mwezini.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


Issa
Alfonso davies dah barca wanamjua huyu mtu muulize semedo
Omary lukumbi
Ni kila kiti kinakua kwa sabab fulan usimdharau mtu usie mjua
Dorophina
Story yake yakusisimua hatari usimdharau usie mjua
Mwajumah
Kweli usimzalau mtu usiyemjua story yake yakusisimua sana#Meridianbettz
aisha
Duuh ana hisitolia nzuri sana ya kujifunza
magdalena
ana historia nzuri sana na kujifunza ni jambo la muhimu sana
Nasra
Inasisimua sana historia yake
Adelta
History yake Ni nzuri ya kujifunza
@meridianbettz
Shan
Kamala safi
Shan
Makala safi
Tatu
Imekuwa history nzuri sana kwake
felister
historia nzuri kuna cha kujifunza
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo vizuri napia anajituma kwenye kazi zake namuerewa kinoma
Neema
Tunajifunza kitu hapa
Ester jackson
Asante kwa nakala
farida ahmadi
Yuko sahihi kabisah
Samiah
Gud
Furahav
Yuko vizuri
Christa
Dahhh, kweli maisha ni safari. Mungu ambariki
Latifa juma mohamed
Hakika maisha ni Safari story inasisimua.