McLaren: Mark Cavendish Atemwa Tena

Mchezaji wa timu ya Bahrain McLaren – mwingereza Mark Cavendish, ametemwa katika orodha ya wachezaji wa timu hiyo watakaoshiriki Mashindano ya Tour de France.

Hii ni mara ya pili kwa Cavendish kutochaguliwa na timu ya Bahrain McLaren kwa miaka miwili mfululizo. Akiwa na umri wa miaka 35, Cavendish ameshinda mara 30 katika Mashindano ya Tour akizidiwa mara 4 na Eddy Merckx aliyeshinda mara 34.

Michuano ya Tour de France imepangwa kuchezwa kuanzia Agosti 29 mpaka Septemba 20 katika jiji la Nice – Ufaransa.

Mapema mwezi wa Mei, kiongozi wa timu ta Bahrain McLaren– Rod Ellingworth alisema Cavendish hakuchaguliwa kwa sababu maandalizi yake hayakuwa mazuri kutokana na mlipuko wa Corona. Cavendish ameshiriki mbio mara 24 pekee msimu huu bila ushindi wowote na mara nyingi amekuwa kama msaidizi wa madereva wenzake.

mclaren
Mikel Landa

Timu ya Bahrain McLaren itaongozwa na Mikel Landa katika Mashindano ya Tour de France. Ellingworth amesema, ” mashindano ya mwaka huu yanamfaa sana Mikel, amekuwa na uwezo ulioimarika zaidi.

“Wachezaji tuliowachagua kumsaidia [Mikel] wanawakilisha wachezaji ambao wapo tayari kwa mashindano haya.”

Orodha ya wachezaji wa Bahrain McLaren kwenye Mashindano ya Tour de France.
  1. Mikel Landa (Hispania)
  2. Pello Bilbao (Hispania
  3. Damiano Caruso (Italia)
  4. Wout Poels (Uholanzi)
  5. Sonny Colbrelli (Italia)
  6. Marco Haller (Australia)
  7. Rafa Valls (Hispania)
  8. Matej Mohoric (Slovakia)

Cavendish alijiunga na Bahrain McLaren kwa makataba wa mwaka mmoja mapema mwezi Oktoba, 2019 na kuungana na kocha wake wa zamani – Ellingworth ambaye aliitumikia timu ya Sky kwa takribani miaka 10.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi Ucheze

20 Komentara

    Usikate tamaa uwez jua wanakuepushia nn

    Jibu

    Asife moyo mzung anasema one day yes.

    Jibu

    Duuh hatari

    Jibu

    Asikate tamaa labda msimu ujao watamchagua tu

    Jibu

    Duuh atari ila asife moyo maana awezi jua wanakuepusha na nn#Meridianbettz

    Jibu

    Kukata tamaa ni zambi

    Jibu

    apambane ili msimu ujao aweze kupata nafasi

    Jibu

    Nafasi bdo ipo akipange kwa msimu ujao

    Jibu

    Uwezo wake ushashuka sasa hivi ukiangalia kuna washiriki wengi chipukizi na wenye vipaji hadi kuimshinda yeye hingekua vizuri haendelee kua kama msaidizi kwa wenzie tu

    Jibu

    Mbona ana uwezo mzuri Sana lakini hawamchukui.. mhhh pengine ana matatizo mengine wanayajua wenyew

    Jibu

    Duuh hatari sana

    Jibu

    Mark Cavendish akuchaguliwavkutoka na maandalizi yake ayakuwa mazuri kutokana ugonjwa wa corona juu ya uwezo aliyokuwa nao

    Jibu

    ajipange tena msimu ujao

    Jibu

    Duu apambane msimu unakuja afanye vizuri

    Jibu

    Uwezo wake ushashuka sasa hivi ukiangalia kuna washiriki wengi chipukizi na wenye vipaji hadi kuimshinda yeye hingekua vizuri haendelee kua kama msaidizi kwa wenzie tu

    Jibu

    Duh nouma Sana ila asikate tamaa

    Jibu

    Ajipange tena uwezo wake umeshuka sana

    Jibu

    Duuh

    Jibu

    Noma sana.

    Jibu

    Duuh hatari sana

    Jibu

Acha ujumbe