Arsenal Wamenionyesha Ufa wa Liverpool

Huenda hatumtazami Mikel Arteta kwa jicho poa, ila ni kocha mmoja wa viwango sana. Hana wachezaji wa kiwango cha juu sana, ila amekazana kuitengeza timu yake ili kupata ubora wa kila mchezaji. Watazame Arsenal walivyokaba kwa nidhamu leo licha ya kutokuwa na wakabaji wazuri. Watazame walivokuwa wanabadilika kwenye ukabaji kwenda kushambulia. Narudia tena, huenda hatumtazami Mikel Arteta kwa jicho poa sana.

Jurgen Klopp anaweza kuwa na msimu mgumu sana kama ataendelea kujiamini na kutokufanya usajili dirisha hili. Mwaka wa tatu huu anakuja na kikosi kilekile. Wametumia nguvu kubwa sana kulipata taji la epl, walitumia nguvu kubwa sana kuipata UEFA, kabla ya hapo bado walifika fainali ya UEFA. Sehemu kubwa ya kikosi cha Liverpool kimechoka kimwili na kiakili. Zinahitajika sura mpya kwa ajili ya kuamsha ari. Sijui kwanini Klopp bado analichelewesha dili la Thiago Alcantara.

Arsenal wameanza huu msimu na mataji mawili. La kwanza ni FA. La pili ni kufanikiwa kumbakiza Pierre Emirick Aubameyang. Yule binadamu anajua, nafasi moja ngumu aliyoipata kipindi cha kwanza ameigeuza kuwa goli. Bado alikuwa muhimu kuziziba njia za Liverpool, bado aliwakumbusha kurudi kila mda kumdhibiti akiondoka kwenye counter attack. Narudia tena, kumbakiza Aubameyang ni kombe lingine la Arsenal.

Nadhani Klopp alimmiss zaidi Trent kuliko uwezo wa Salah. Liverpool hawakuwa hatari kabisa upande wa kulia, kibaya zaidi ni upande huo hatari za Arsenal zilipotokea. Salah alikuwa siku mbaya sana ofisini, ila haikuwa bahati mbaya. Kiran Tierney alishuka nae kiume.

Labda ni mimi tu nimemuona ukuta wa Liverpool ukicheza juu kuliko kawaida. Labda ni mimi tu nimevutiwa na utulivu wa Mohamed Elneny, labda ni mimi tu nimevutiwa na mizunguko ya Bukayo Saka. Labda ni mimi tu nimeiona mikono ya Emilano Martinez. Labda ni mimi nimewaza haya. Labda ni mimi tu.


Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

47 Komentara

    Kweli arsenal wameonyesha uwezo wao ; pongezi kwa Arteta ni kocha mwenye uwezo

    Jibu

    Arsenal jana walicheza mpira wa kiwango kizuri sana pongezi kwao

    Jibu

    arsenal jana wametudhiriishia kuwa wapo bado wapo kwenye kiwango

    Jibu

    Pongezi sana kwa Arsenal Jana walijua kucheza sana mpira wa kiwango Cha juu#Meridianbettz

    Jibu

    Arsenal Mambo Ni Moto!!

    Jibu

    Arsenal wako vizuri sana

    Jibu

    safi sana arsenal kuwa na mwanzo mzuri

    Jibu

    Arteta ni kocha mwenye viwango

    Jibu

    Kwa upande wangu kwa Liver bado naona wapo vizuri sana ila kwa upande wa Arsenal Arteta anatakiwa afanye kitu kwenye usajili ili kuboresha kikosi chake zaidi kwenye sehumu mbili tatu ikiwemo Winga zone

    Jibu

    Congrat The gunners🤝🤝🤝

    Jibu

    Arsenal wamekuja kwa kasi

    Jibu

    Ahsanten arsenal mnatuonyesha ubora wenu.

    Jibu

    Safi arsenal

    Jibu

    Safi sana arsenal

    Jibu

    Vizuri Sana Arsenal kwakumpiga Liverpool kwamikwaju ya penati Mambo yalikuwa vizuri kwao

    Jibu

    Arsenal walifanya vizuri sana

    Jibu

    Baada ya Arteta kuchukua mikoba ilishinda dhidi ya vigogo EPL na kwakuwa msimu ujao ataanza na timu kuanzia mwanzo bila shaka atatuonyeshakitu cha tofauti, tutarajie surprise#meridianbettz

    Jibu

    Uwezo wa Arsenal kwa sasa ni mzuri

    Jibu

    Ni swala la muda na usajili ndo anachohitaji Arteta ila ana uwezo mzuri

    Jibu

    Ahsanteni Arsenal kwa kunifurahisha jana mlicheza mpira

    Jibu

    Liver team zimeshajua uzaif wao

    Jibu

    Nice arsenal

    Jibu

    Pongezi Sana arsenal

    Jibu

    Arsenal mmekiwasha vya kutosha!!!

    Jibu

    Arsenal Level imeanza kurudi

    Jibu

    Arteta ni kocha mzuri sana.

    Jibu

    Arsenal Jana wamenikoshaaa.

    Jibu

    Arsenal mmejua kunipa raha

    Jibu

    Hii ndo maana ya kusajili nategemea mazuri kutoka arsenal

    Jibu

    Arsenal haki ya nani wametishaa

    Jibu

    habar njema

    Jibu

    Arsenal wasilewe sifa bashabiki wanataka kuona mengi mazuri na sio kuishia hapo tu

    Jibu

    Nihabar njemaa

    Jibu

    Kwa mwenendo huu inaonesha arteta anaweza akafit arsenal.

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Arsenal jana wamecheza vizuri sana na siku zote liverpool kwenye upande wa penarty hua awapo vizuri

    Jibu

    Asanten kwa taarifaa

    Jibu

    Arsenal msimu huu watatisha

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Kocha kloppa ameona kiti cha moto kwa arsenal ndiyo ajue kwamba kupata kombe kwa zaidi ya miaka 30 sio kwamba amemaliza

    Jibu

    Pongezi ziende kwa arsenal

    Jibu

    Arsenal kiwango chao kizuri sana

    Jibu

    Wamejitahidi sana

    Jibu

    Wamejitahidi wazidi kujipanga vizuri zaid hongeren sana#meridianbett

    Jibu

    arteta kazi kubwa ya kukisuka kikosi cha arsenal kaifanya anastahili pongezi kubwa sana

    Jibu

    Kwa upande wangu kwa Liver bado naona wapo vizuri sana ila kwa upande wa Arsenal Arteta anatakiwa afanye kitu kwenye usajili ili kuboresha kikosi chake zaidi kwenye sehumu mbili tatu ikiwemo Winga zon

    Jibu

    Arsenal Emirates jeshiii

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.