Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amefunguka kwamba straika wake, Meddie Kagere anakaa benchi kutokana na yeye kupanga na kuchagua timu kutokana na aina ya timu ambayo anaenda kukutana nayo kwenye mechi zao.
Kocha huyo ameongeza kwamba pia amekuwa akiangalia zaidi mafanikio ya timu yake katika kushinda na wala siyo mtu mmoja huku kila mchezaji aliye hapo anaweza kukaa benchi kutokana na atakavyokuwa anawaona wapinzani wake.

Kagere ambaye alikuwa mfungaji bora wa timu hiyo kwa msimu uliopita, amekuwa akikosa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ikiwemo katika mechi ya Ngao ya Jamii mbele ya Namungo FC ambapo Simba walishinda mabao 2-0.
Sven amesema kwamba hakuna tatizo la Kagere kukaa benchi ndani ya timu hiyo kutokana na hali hiyo inaweza kumkuta mchezaji yeyote ndani ya kikosi hicho kwa sababu ya kuangalia mafanikio zaidi ya kikosi hicho kuliko mtu binafsi.

“Kuhusiana na Kagere wala hakuna tatizo lolote lile la yeye kukaa benchi kwa sababu hilo linaweza kumtokea kila mchezaji aliye hapa.
“Nachagua timu kutokana na mfumo ulivyo na namna tunavyocheza, sijui kwa nini watu wanazungumzia kuhusiana na mtu mmoja.
“Naangalia mafanikio zaidi ya timu, kama tunashinda iwe timu na hata tukipoteza ni kwa ajili ya timu na hata tuchukue mataji ni timu, siyo mtu mmoja.
“Lakini vilevile anaweza kutumika kwenye mechi zetu zinazokuja mbele na wengine wakakaa tu nje,” alimaliza Mbelgiji huyo.
SHINDA NA HI LO
Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.


Povel
Sawa sven kocha wa mabingwa wa nchi na tumekuelew THis is SIMBA next level
felister
Sven yupo sahihi yeye anachoangalia ni mafanikio ya timu na siyo mtu
magdalena
maamuzi ya kocha ni mazuri sana kwa ajili ya manufaa ya timu ila tatzo linakuja pale watu wanapozusha maneno ya sintofahamu
Zeiyana
Kagere hana mahajabu tena na ndio maana kocha amekua hana hunakini nae mwisho wasiku utasikia tu kagere kauzwa
Adelta
Tumekuelewa kocha Steve@meridianbettz
Janeflora malisa
Ni vzr
Sauda
Kocha yuko sahihi kabisa
Tatu
Kocha yupo sahihi watu wasilete maneno maneno yeye anachoangalia nani anafanya vizuri msimu huu nani apumzishe yupo kwa ajili ya kikosi kizima
Caroline
Mnatuficha tu .Ila mbona za chini ya kapeti tunasikia kagere alimpiga kocha😂😂😂😂😂
Shani
Mahamuzi ya koch yaeshimiwe juu yy anawatambua vyema vijana wake!!
Mwanahamisi
Safi sana
Mwajumah
Kagere hana jipya ndio mana kawekwa benchi hana maajabu simkubal wala nn#Meridianbettz
Dorophina
Kagere ameanza taratibu mwisho wa siku atasema anataka kuama mchezaji anamaamuzi gani ya kuchagua mechi ipi anayotaka kuchezea
Ernest
Approach ya Kocha Sven ni nzuri lakini moja kwa moja inamuathiri Kagere kwa kiasi kikubwa sana hasa ukiangalia kwa misimu takribani miwili amekuwa mfungaji Bora lakini kwa upande mwingine nadhani Mwalimu anataka kumjenga zaidi kisaikolojia Kagere baada ya sekeseke lake la power Bank kwani wengi tunaona alishuka kwenye kufumunia Nyavu.
Devotha
Akae tu benchi siku hizi hana maajabu
Nasra
Itamsaidia kujipanga vzuri tena
Fatina mfigi
Kagera Ana maajabu kma zamani!
Elika
Kocha upo vizuri
aisha
Oky kocha sven naamini mambo yatakua mazuri zaidi maana sisi wana simba tunachotaka ni ushindi
lombo
Simba next level
Lydia Emmanuel Magoti
Alichokisema kocha kipo sahii kagere sio Kama apangwi kocha anakili yake awezi kuwachezesha viungo hote kipindi chakwanza ndomana kocha anamwanzisha Boko kagere mmaliziaji Sasa yeye kagere anataka kuchezeshwa ote kipindi kimoja Sasa kocha amegutuka Sasa ivi amebadiri utandawazi ndomana ana muanzisha moja moja ana malizia Sasa kagere ana ona Kama apangwi ana wekwa benchi Sana ndomana anapaniki
Flomena
Naangalia mafanikio zaidi ya timu, kama tunashinda iwe timu na hata tukipoteza ni kwa ajili ya timu na hata tuchukue mataji ni timu, siyo mtu mmoja.
Saupha mohamed
Sawa tu tunachoitaji kikosi kizuri
Shafii
Kila kocha hua anamfumo na mbinu zake kwaiyo anajua aina gani ya wachezaji akiwatumi watafanya vile anachokitaka.
farida ahmadi
Yuko sahihi kabisah Steven
JULIANA WILBARD ALEX
Wapi Kagere Kagere
Amiri Kayera
Wachezaji wot wazur na uwez kuchezesh wote lazm wengne wakae benchi
Sadick
Kauli ya Sven inaongeza tetesi kwamba wawili hao walikunjana hivi karibuni,pengine anajaribu wachezaji wengine waliosajiriwa hivi karibuni#meridianbettz
Latifa juma mohamed
Lakini vilevile anaweza kutumika kwenye mechi zetu zinazokuja mbele na wengine wakakaa tu nje,”
Hope mwaikuka
Umeeleweka kocha
Issa
Kagere hana jambo umri umesogea
Genia Sikaluzwe
Lakini vilevile anaweza kutumika kwenye mechi zetu zinazokuja mbele na wengine wakakaa tu nje,”
David Pere
Approach ya Kocha Sven ni nzuri lakini moja kwa moja inamuathiri Kagere kwa kiasi kikubwa sana hasa ukiangalia kwa misimu takribani miwili amekuwa mfungaji Bora lakini kwa upande mwingine nadhani Mwalimu anataka kumjenga zaidi kisaikolojia Kagere baada ya sekeseke lake la power Bank kwani wengi tunaona alishuka kwenye kufumunia Nyavu.
Isaya massawe
Wamwache kocha afanye yake
Khadija
hayo ni maamuzi yake kocha ss mashabiki yetu macho#meridianbettz
Rehema
Bonge la makala
Sabrina
Kazi na umri
Ester jackson
Tumetoka kwa bale sasa kwa kagere
warda
Sie Tunataka ushindi tu Mengine Atajua mwenyewe
Tahiya
Tumuache kocha hafanye kazi yake
Furahav
Kocha yuko sahii.
Samiah
Yupo sahihi Kocha