Xavi na Iniesta Walivyonionyesha Ajabu Lingine la Dunia

Hadi Sir. Alex Ferguson alinyoosha mikono juu na kukiri kwamba amewashindwa. Wakati Barcelona wanaibutua Man United katika fainali ya UEFA mwaka 2011 pale Wembley, shoka Iniesta na mpini wake Xavi walimsimamia kooni. ‘Big g’ zake zikawa chungu. United walipiga shuti moja tu lilolenga lango, walikuwa na umiliki wa mpira wa asilimia 33 tu. Walizidiwa kila kitu na Barca kasoro kadi na rafu tu.

Baada ya mchezo Fergie alisema “Sijawahi kucheza na timu ngumu kama hii. Timu iliyokamilika kila eneo kama hii, sijawahi kuiona. Sijawahi kukutana na viungo wanaoelewana kama hawa. Kuna muda nilidhani wachezaji wangu wataanguka kwa kizunguzungu kwa namna mpira ulivokuwa unazunguka. Yule Xavi na Iniesta walitushinda ujanja kabisa.” Kumbuka hapo Barca walikuwa wanaipiga United kwa mara pili mfululizo katika fainali ya UEFA.

Kwasababu tupo na Xavi leo, tumuache huyu ndugu yake. Tutamrudia Iniesta siku nyingine. Xavi yeye alifika Barcelona mapema sana, akiwa na miaka 11 tu alijiunga na ‘La Masia’. Kwasababu alitokea katika familia bora kifedha, hakuwahi kulazimishwa kwenda shule. Wazazi wake walimshauri aweke nguvu zaidi kucheza mpira kuliko kusoma, walimuona akifanikiwa zaidi ndani ya uwanja kuliko darasani. Wakampeleka La Masia akaanze maisha ya soka.

Alikulia hapo akizitazama sana mechi za kingereza. Yeye mwenyewe anadai kuwa analihusudu sana soka la Paul Scholes. Basi akakulia katika academy ya La Masia. Alipokuwa na miaka 19, AC Millan walitaka kumsajili. Wakamuahidi mshahara mrefu na nafasi katika timu ya kwanza. Kumbuka enzi hizo AC Millan wanatesa Ulaya. Xavi alikuwa tayari kupokea hiyo ofa, baba yake vilevile alikubali. Ila mama yake alimuambia akiondoka Barcelona atavunja ndoa na baba yake. Waachane. Basi Xavi kwa kuiheshimu ndoa ya baba akaamua kubaki Barca.

Ni mume wa Nuria Cunirella, msichana aliyemgombania na Carles Puyol mwaka 2012. Puyol aliachana na mpenzi wake ili awe na Nuria, ila Xavi alimzunguka na kumpata Nuria. Walipofunga ndoa 2013, wachezaji wengi wa Barca walihudhuria ila Puyol hakuwepo. Mpaka leo inadaiwa hawana mahusiano mazuri. Mapenzi bwana!


SHINDA NA HI LO

Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.

Cheza sasa

40 Komentara

    Thnks meridian ilikuwah combination nzur Sana dimba la Kati na nilikuwah kizaz cha dhahabu Kwan walifanikiwah kutwaaa makombe yote yaliyokuwah mbele yao thnks meridian kwa update

    Jibu

    Xavi na Iniesta ni balaa lingine kwenye ulimwengu wa soka nadhani historia yako itadumu kwa muda mrefu.

    Jibu

    hawa vijana ni moto wa kuotea mbali wanajua sana tena sana

    Jibu

    Hayo jamaa wapo vizuri hawataki masihara kabisa

    Jibu

    Xavi na inista Ni vijana wenye uwezo mzuri kwa ulimwengu wa soka
    @meridianbettz

    Jibu

    Vijana wanajua hadi wamepitiliza

    Jibu

    History yao nzr sana

    Jibu

    hawa jamaa si watu wa mchezo mchezo

    Jibu

    Ki ukweli xavi aliupenda sana mpira ndio maana kipindi hanapo kua uwanjani hanacheza mpira kutoka moyoni..!

    Jibu

    Xavi na Iniesta ni moto wa kuotea mbali hakika wamecheza mpira mzuri

    Jibu

    Xavi na lniesta ni jeshi kubwa akuna wa kupiga hili!

    Jibu

    Historia yao nzuri

    Jibu

    Historia nzuri

    Jibu

    Yess ndivyo wachezaji wanatakiwa kuwa.

    Jibu

    Jamaa wapo vizur sana sio watu wa mchezo mchezo#Meridianbettz

    Jibu

    Vzuri sana kwa hao jamaa

    Jibu

    Miamba miwili hiyo naikubali sanaaa

    Jibu

    Hawa vijana wako vizuri

    Jibu

    saf

    Jibu

    Hawa jamaa nawakubali kinoma Sana wanajua wapambanaji

    Jibu

    Baada ya mchezo Fergie alisema “Sijawahi kucheza na timu ngumu kama hii. Timu iliyokamilika kila eneo kama hii, sijawahi kuiona. Sijawahi kukutana na viungo wanaoelewana kama hawa. Kuna muda nilidhani wachezaji wangu wataanguka kwa kizunguzungu kwa namna mpira ulivokuwa unazunguka. Yule Xavi na Iniesta walitushinda ujanja kabisa.” Kumbuka hapo Barca walikuwa wanaipiga United kwa mara pili mfululizo katika fainali ya UEFA.

    Jibu

    Vijana wapo vizurii

    Jibu

    Wadau wa soka tukiwaona hawa jamaa tunakumbuka ile fainali ya club bingwa 2011 jinsi gani walimfanya sir Alex kutetemeka Kama kapigwa short.

    Jibu

    Wanahistoria nzuri Sana

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Walikua bola San kipindi chao

    Jibu

    Xavi na Iniesta walitengeneza Chemistry bora kuwahi kutokea duniani#meridianbettz

    Jibu

    Hao watu ni nomaaa

    Jibu

    Good newz

    Jibu

    Viungo ambao hawajawahi kutokea spain

    Jibu

    History zuri sana

    Jibu

    Thnks meridian ilikuwah combination nzur Sana dimba la Kati na nilikuwah kizaz cha dhahabu Kwan walifanikiwah kutwaaa makombe yote yaliyokuwah mbele yao

    Jibu

    Wajamaa wana hatari hawaaaa

    Jibu

    hawa vijana wanajua sana#meridianbettz

    Jibu

    Xavi na Iniesta sio poa wanabalaa zito kwenye soka

    Jibu

    Asante kwa nakala

    Jibu

    Namwonaga Xavi na Iniesta hawana bahati kabisa

    Jibu

    Habari nzuri.

    Jibu

    Safi

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.