Bella Gutaman, gwiji fulani wa Benefica aliwahi kusema “mfumo au falsafa haiwezi kutamba kwa zaidi ya miaka minne.” Gutaman alisema hivo kwasababu anaamini mfumo wako unapofanya vizuri, timu pinzani zinaumiza kichwa kukusoma na suala la muda tu kabla hawajapata mbinu za kukuvuruga.
Liverpool chini Jurgen Klopp, imeishi kwa kutegemea ubora wa wachezaji watano kuwapa magoli. Mabeki wawili wa pembeni na washambuliaji watatu. Wanategemea zaidi kupita pembeni na kutengeneza nafasi kutokea pembeni. Kazi kubwa ya viungo wa Klopp ni kukaba mpira na kuuepekela pembeni, huko ndipo mabao yanapopikwa. Usishangae ukiambiwa ‘full backs’ wa Liverpool wanaongoza kwa assist ndani ya Liverpool.

Kwa falsafa hii, Liverpool wamebeba taji la ligi(EPL) na Ulaya(UEFA). Kama uliwatazama Liverpool walipocheza na Leeds mchezo wa ufunguzi, nadhani uliona namna vijana wa Marcelo Biesla walivopambana kuwazuia mabeki wa pembeni wa Liverpool. Na hii inakuwa mara ya kwanza Liverpool kufunga mabao 3+ bila beki wao yoyote wa pembeni kutoa assist kutoka kwenye mchezo wa wazi (open play).
Hii inamaanisha nini? Huenda ukawa mwisho wa ujanja wa Klopp kushinda kirahisi kutokea pembeni. Ameshatesa sana na hii falsafa, sasa ni muda wa kubadilika na kujaribu kitu kingine kipya.
Hiki kitu kipya anakuja nacho Thiago Alcantara, kwa muda mrefu Liverpool haijawa na viungo wabunifu na wamiliki mpira. Labda ndio sababu iliyomfanya Klopp ategemee zaidi upishi kutokea pembeni kuliko katikati. Uchezaji wa Thiago unakuruhusu kupita katikati ya uwanja. Ni aina ya mtu anayejua kusambaza mpira. Japo hatakupa sana pasi za mwisho, ila atakufikishia mpira hadi mpigaji wa pasi ya mwisho. Nadhani ni muda Klopp anaenda kubadilika na kujaribu kucheza katikati ya uwanja zaidi ya pembeni.
![]()
Thiago ataitoa timu nyuma ataifikisha mbele, wale washambuliaji watatu wa mbele watakuwa na kazi mbili. Kwanza kutengenezeana nafasi na kufunga. Hii itampa ahueni Firmino, aliyelazimishwa kushuka chini ili aisaidie timu kucheza. Ndiyo maana alikaukiwa mabao msimu uliopita. Kwasababu Thiago atakuwa mchezeshaji, yeye atabaki juu na jukumu lake mama la kufunga na kupika mabao.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Mariam mtandama
Habari njema
felister
hayo ni maneno tu wanamkatisha klopp tamaa
Tatu
Thiago amekuja kufanya mabadiko Liverpool msimu huu
Dorophina
Liver lazima na msimu huu wabebe hizo Ni hisia za wapenzi watazamaji hazitasaidia chochote
Faraja molell
Thiango anajituma sana
Lydia Emmanuel Magoti
Wanamkatisha Kropp tamaa ila akipambana anaweza
Zeiyana
Klopp yupo vizuri sana hanambinu nyingi
Sadick
Mpira ni sayansi ya mbinu na falsafa ya Pep Guardiola haijawahi kubadilika na anapata matokeo mazuri#meridianbettz
Devotha
Klopp ni kocha mzuri sana
Rehema
Ni kocha mzuri sana klopp
jullie
yuko vizuri jamaa
Antony Luseno
Mtazamo wa Gutaman upo sahihi sana na ni wa kuheshimiwa
caroline
anamaanisha mfumo anaotumia klopp sio mzurii
Nasra
Klopp yuko vzuri
Mwajumah
Ni kocha mzuri sana klopp#Meridianbettz
Angelina
Klopp yuko poa
Sauda
Ni kocha makini sana
Adelta
Klopp Ni kocha mzuri@meridianbettz
Ernest
Ngoja tuone mwisho wake
aisha
Kwa ligi ya uingereza kutamba miaka miwili ni kitu kigumu sana
Hidaya
Klopp anajua anachokifanya
Gabriel
Klopp ni kocha mzuri
Khadija
Klopp yupo vzr#meridkanbettz
Hopemwaikuka
Yote yanawezekna Ila akipambana anatamba tu hata miaka kumi
Issa
Ni ngum epl ligi ya ushindan
Amiri Kayera
Kwa kocha kufanya vizur Kwa mda mlef team moja ngum
Saupha mohamed
Good news
JULIANA WILBARD ALEX
Anajua
Povel
Ngoj tuone final itakuwaje
Neema
Klopp yuko vizuri
Theonestina
Namkubar
David Pere
Kwa ligi ya uingereza kutamba miaka miwili ni kitu kigumu sana
magdalena
klopp yupo vizuri sana ila kila kukicha anabidi abuni mbinu mbadala kwa ajili ya timu
warda
Ni kweli kabisa
Fatina
Safi
Tahiya
Hata ivyo amefanya mambo makubwa kwa kila klabu aliyofundisha
Salma ngende
Bado yupo vizuri
Shan
Epl ni iigi ya upinzan kudum na title mfululizo haliwezekan
Sabrina
Klopp yupo vizuri inabidi aendelee kukaza