Kabla Sijamlaumu Maguire, Nataka Nikutane Ed Woodward

Arsene Wenger aliwahi kusema zipo njia mbili tu za kutengeneza timu imara ya ushindani. Ya kwanza ni kuwekeza katika kukuza vijana na ya pili ni kumwaga pesa kununua waliokwisha kutengenezwa. Njia zote hizi zinafanya kazi lakini hazifanani.

Njia ya kwanza inahitaji uvumilivu na mipango ya muda mrefu sana. Ndiyo sababu timu nyingi zimepiga chini huu mpango. Wanachagua tu kujitosa sokoni na kutengeneza timu imara. Ndivyo pesa inavyoendesha dunia. Kuanzia kwa Real Madrid iliyotwaa UEFA tatu mfululizo mpaka kwa PSG na Bayern Munich zinazocheza ligi zao binafsi, zimeundwa kwa pesa tu. Hakuna kingine!

Kwa Manchester United, kabla ya kuilaumu mikono ya David De Gea, kabla ya kuzihoji mbinu za Ole Gunner Solksjaer, kabla ya kuzituhumu kosakosa za Antonio Martial, nadhani anatakiwa kutazamwa Mkurugenzi Ed Woodward na ‘sekretarieti’ yake. Kwa walipoishia Man United msimu uliopita, ni wazi walihitaji sura mpya kikosini ili kupiga hatua zaidi. Walihitaji marekebisho baadhi ya maeneo ili kuwa washindani zaidi.

Sahau kuhusu ulinzi, kule mbele wanahitaji washambuliaji wawili hatari (siyo machachari), watu kama Harry Kane na Jadon Sancho. Katikati walifanya vizuri kumuongezea Bruno msimu uliopita na ujio wake umelipa, tayari wanayo Pogba, Fred, Mctominay na Matic. Kwa maoni yangu nadhani katikati hawahitaji mtu ukizingatia wamemsajili Donny Van Beek. Wanahitaji beki mmoja wa kati wa kusimama na Maguire na beki mmoja wa kushoto. Hao tu.

Hayo maelezo niliyoweka hapo juu, nimerudia tu alichokisema Ole mwisho wa msimu uliopita alipozungumzia marekebisho atakayofanya kikosini. Ajabu ni kuwa hajayafanya mpaka sasa. Unadhani shida ipo wapi? Shida siyo Ole, shida ni mtu anayesimamia fedha, Ed Woodward. Hakuna kocha asiyetaka kusajili, hakuna kocha asiyetaka kushinda. Kama Ole aliona madhaifu yote hayo, ina maana alihitaji kuyarekebisha. Atarekebisha vipi bila pesa ya usajili?

Crystal Palace walivoshuka Old Trafford jana bila uwoga, Man Utd inahitaji kufanya kitu kabla dirisha halijafungwa kama kweli wanahitaji taji la ligi kuu.


SHINDA NA MERIDIANBET!

Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.

Cheza Sasa.

37 Komentara

    Maneno aliyosema arsene wenger ni mnzuri Sana vilabu vingi vingefuta mfumo wake wala wasingepoteza pesa nyingi kwenye usajili

    Jibu

    Ukingalia ni kweli man chester wanaitaji wachezaji machachali na wanao jituma sain ya Sancho ndio ingekua bola kwao

    Jibu

    Wenger yupo sahihi kwa alichokiongea man u kwa sasa inahitaji kikosi kizuri na watu wanaoujua mpira vizuri ili kuiinua klabu

    Jibu

    Nikweli man wanaitaji wachezaji wenye kujituma na wenye judi zakupambana kwaio inabidi wafanye usajiri kwaraka kabla dirisha alija fungwa wa pate majembe wenye amsha masha ya timu

    Jibu

    Man United bado wanakikosi kibovu tu

    Jibu

    Ferguson alipata mafanikio makubwa hata wakati timu haikuwa na wachezaji wazuri sana alijua namna ya kuwapa motisha na kufuata game plan. kwa sasa Man U tatizo ni kocha pia#meridianbettz

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    habari nzuri

    Jibu

    United wasipo pata ufumbuzi ni wapi wanafeli itawagharimu ata zaidi ya miaka 15 pasipo kuchukua kombe la EPL

    Jibu

    man u wanatafuta wa kumtupia lawamaa

    Jibu

    Man u wajipange upya

    Jibu

    Man u bado wanakikosi kibovu sana wasitafute mtu wa kumpa lawama#Meridianbettz

    Jibu

    Man U wanatakiwa kuimarisha kikosi

    Jibu

    🔥🔥

    Jibu

    man kwa sasa imekua jumba bovu

    Jibu

    Old Traford patachimbika pale we subiri

    Jibu

    United inabid isajili washambuliaj makin wa kutupia ili isake ubingwa tena

    Jibu

    Man u wajipange upya waangalie wapi walipokosea

    Jibu

    vilabu vingi vingefuta mfumo wake wala wasingepoteza pesa nyingi kwenye usajili

    Jibu

    Asante kwa nakala#meridianbettz

    Jibu

    Na hii ndio sababu ya kufkr kabla ya kutenda

    Jibu

    Ole ana kikosi imara sana ila mbinu tu aongeze

    Jibu

    Man U sijajua tatz wapi

    Jibu

    United wamestail walichokipata ukiangali ah mchezo wa jana wamecheza chin ya kiwango wachezaj wote wanapaswa kulaumiwah

    Jibu

    Man U kikubwa kukaa kutuliza kichwa kwanza

    Jibu

    Man mnatuangusha Sana bwana

    Jibu

    Man waimarishe kikos

    Jibu

    Ferguson alipata mafanikio makubwa hata wakati timu haikuwa na wachezaji wazuri sana alijua namna ya kuwapa motisha na kufuata game plan. kwa sasa Man U tatizo ni kocha pia

    Jibu

    wenger alikuwa anatazama mbali sana

    Jibu

    Swala la kukuza vijana ndo muhimu sana#Meridianbettz

    Jibu

    Man u wanatuangusha

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Man u wajipange

    Jibu

    Man u bado wako vibaya

    Jibu

    Sijui man wanakwama wapi siku hiziii

    Jibu

    Ni umakin tu na kufanya usajili kwa fowad matata tu na idara ya ulinz

    Jibu

    Man u wanatakiwa wajipange wana kikosi kibovu

    Jibu

Acha ujumbe