Ansu Fati Asaini Dili ya Miaka 4 Barcelona.

Barca na Ansu Fati wamefikia makubaliano ya kuboresha kandarasi ya mchezaji huyo hadi Juni 30, 2024, na kifungu chake cha kuondoka kikipanda kutoka € 170m hadi € 400m.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 17 amekuwa mmoja wa nyota waliowika sana Ulaya msimu uliopita na anatajwa kuwa na mustakabali mzuri huko Barcelona.

Kinda huyo alifungia Barca mabao 8 msimu uliyopita na aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Spain na kufanikiwa kufunga mara mbili kumuweka katika nafasi nzuri Spain ilipoifunga Ukraine 4-0 mapema mwezi huu.

Amekosa michezo miwili ya kwanza tangu Koeman achukue mikoba ya kuinoa Barca, kutokana kuwa na majeraha, Fati alianza katika mchezo wa kirafiki wa Joan Gamper Trophy dhidi ya Elche .

Maboresho ya mkataba wa Ansu Fati na  Barcelona.

Kifungu cha awali kwenye Mkataba wa Kinda huyo kilikuwa €100m kikapanda hadi €170m na yakawekwa makubaliano kwamba wakati mchezaji huyo atakapo ingia rasmi katika kikosi cha kwanza cha Barça kifungu kitaboreshwa hadi euro milioni 400.Euro milioni 400 Kumwondoa Ansu Fati Barca!

Winga huyo amekabidhiwa jezi namba 22, ambayo ilikuwa ikivaliwa na mchezaji Artulo Vidal ambaye ametimkia Inter Milan wiki hii.

Kabla alikuwa akivalia jezi yenye namba 31, lakini hakuwa mchezaji rasmi wa timu ya kwanza licha ya kucheza michezo 33 katika mashindano yote msimu 2019-20.

Barca ambao wapo katika marekebisho ya kikosi chao,na wataanza mbio za kuwania LaLiga siku ya Jumapili kwa mchezo dhidi ya Villarreal, wameruhusu Vidal, Arthur,Nelson Semedo na Ivan Rakitic kuondoka klabuni hapo, uhamisho wa Suarez kwenda Atletico Madrid umekamilika imebaki kutia saini tu.


FURAHIA KASINO YA MTANDAONI

Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.

Cheza Sasa

39 Komentara

    Barca wameula…

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Big deal kwake ansu fati mkwanja mrefu sana huo

    Jibu

    Ansu ni hazina kubwa sana kwa Barca

    Jibu

    Good 👍

    Jibu

    Hongera sanaaa

    Jibu

    Goodnews

    Jibu

    safi sana fati fanya kazi kijana ili utoke na historia nzuri apo

    Jibu

    Vizuri sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Kipengele kama hiki ndio ndicho kilifanya PSG kulipa hela nyingi kumnunua Neymar#meridianbettz

    Jibu

    Big up

    Jibu

    Gud

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Pongezi kwa Ansu tunataka kuona maajabu yako

    Jibu

    Vzr

    Jibu

    Barcelona wamepata jembe

    Jibu

    Good kwa barcelona maana inawabidi waimarishe kikosi wasije kutia aibu ya msimu ulioisha

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Wamejipatia jembe

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Back wamepata jembe kwenye umri mdogo hongera zake# merdianbett

    Jibu

    Deal done

    Jibu

    Ni kijana anaechipukia Kwa kasi zaid

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

    Deal done

    Jibu

    Imekaa poa sana 👍 kwa Ansu tunataka kuona maajabu yako wamepata jembe kwenye umri mdogo

    Jibu

    Hongera zake

    Jibu

    Barcelona wanaitaji wachezaji wachanga wenye kujituma ili kuweka timu yao kwenye ubora

    Jibu

    Bonge la dili!!

    Jibu

    Ni mwanzo mzuri wa ansu fati

    Jibu

    Kwa raha zake

    Jibu

    mwanzo mzuri kwa ansu

    Jibu

    Good kwa barcelona maana inawabidi waimarishe kikosi wasije kutia aibu ya msimu ulioisha

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.