Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anaamini Barcelona bado wana kikosi kinachoweza kupambana kwa kila mashindano.
Baada ya kuumaliza msimu bila kuambulia taji lolote, Ronald Koeman anakazi kubwa ya kuijenga Barca, ambao tumeona wakiuza wachezaji wao Luiz Suarez, Arturo Vidal,Ivan Rakitic, Arthur na Nelson Semedo.
Philippe Coutinho amerejea kutoka Bayern Munich ambako alitumia msimu mmoja kwa mkopo na Miralem Pjanic ametua Camp Nou akitokea Juventus wakati Messi pia ataendelea kuhudumu Barca baada ya jaribio lake la kutaka kuondoka kugonga mwamba.
Zidane, ambaye atawatembelea Real Betis siku ya Jumamosi, amesema Barca bado ipo imara katika kuleta changamoto ya kuwania taji.

“Nitaheshimu upande huo, sijui ni nini kinaendelea ndiyo maana sitaki kujihusisha. Kocha Zidane aliongea na waandishi wa habari.
“Nadhani kila klabu ina magumu yake na mambo yake, nadhani Barcelona kwa dhana ya timu na kikosi itaendelea kupambana kwa kila kitu.
“Sina shaka yoyote.
Lakini pia tumeona baadhi ya mabadiliko katika kikosi cha Real Madrid kwa kuwaachia wachezaji Jmaes Rodriguez aliyetimkia Everton, Gareth Bale akirejea katika timu yake ya zamani Tottenham kwa mkopo na Reguilon ambaye pia amejiunga na upande wa Jose Mourinho.
Mahusiano ya Bale na Zidane iliripotiwa kutokuwa mazuri kwa miezi ya hivi karibuni na mchezaji huyo kutoka Wales amesema kamwe hatojutia kuondoka Madrid.
Alipoulizwa anachochote cha kuongea kuhusu Bale, Zidane alijibu: “sitaongea chochote kuhusu Gareth Bale zaidi tunamtakia kila la kheri.
FURAHIA KASINO YA MTANDAONI
Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.


Mwajumah
Anachosema Zidane ni sahihi kwan barca wanakikosi kizuri tu wajitaidi kwenye mazoezi ili kupata matokeo mazuri msimu ujao na si kama walivyomaliza msimu kwa kutopata taji lolote
Fatina mfigi
Ndio kikosi bado kizur kikubwa kufanya mazoezi kwa bidii na kumsikiliza kocha mbon watapat matokeo mazuri
felister
kikubwa ni mazoezi wakijitahidi barca wataweza kufanya vizuri msimu huu
Nasra
Waongeze ujuzi tu barca wapo vzuri
Caroline
Kikosi cha Barcelona kipo vizuri
Lydia Emmanuel Magoti
Yangu macho ngoja tuone
Zeiyana
Barcelona bado kabic wanaitaji wachezaji wenye uwezo ili kufanya kikosi chao kiwe na ubora
Antony Luseno
Sidhani kama kuna mtu yupo wa kukibeza kikosi cha barca pamoja na kutopata matokeo mazuri kwa baadhi ya mechi
Adelta
Kikubwa wajitahidi na mazoezi
aisha
Wanatakiwa tuu waongeze jitihada ili mambo yakae sawa
Saupha mohamed
Apo wapambane na mazoezi
Tatu
Kikosi cha barcelona bado sana naona wao wanamtegemea sana mess koeman hana kazi kubwa kuunda kikosi na kukiweka sawa
Hopemwaikuka
Ni kweli waongeze juhud tu
Shani
Zidane anaona karibu na ni hofu tu ila sidhan kama Kikosi cha barca kile cha iniesta xavi mbele gaucho etoo kitatokea tena
Elika
Ngoja tuone
Gabriel
Kikosi cha Barcelona kipo vizuri
Amiri Kayera
Barcelona walivulugw na matokea ya last season
Ernest
Ngoja tuone sijui kama kuna maajabu yoyote
Sadick
Barcelona na Real Madrid zote mbili hazina vikosi shindani msimu huu naona Atletico pekee ndio imejipanga kuleta ushindani#meridianbettz
Issa
Hayo ni maneno ya uoga tu sidhan kama barca ipo onfire
Samiah
Ngoja tuone matokeo
Latifa juma mohamed
Nadhani kila klabu ina magumu yake na mambo yake, nadhani Barcelona kwa dhana ya timu na kikosi itaendelea kupambana kwa kila kitu.
David Pere
Ndio kikosi bado kizur kikubwa kufanya mazoezi kwa bidii na kumsikiliza kocha mbon watapat matokeo mazuri
Rose kapinga
Wafanye juhudi tuu,kikosi kiko vizuri tuu
Sabrina
Barca wapo vizuri
magdalena
barcelona kweli bado wana kikosi kizuri ila wanabidi wakiimarishe zaidi ili kiwe kizuri zaidi kama zamani
Dorophina
Barca wanakikosi kizuri kweli sijui hata wanakwama wapi
Povel
Ngoj tuone msimu huuu
Tahiya
Ligi ndio kwanza imeanza