Mfungaji namba moja ndani ya Bongo kwa misimu miwili mfululizo akiwa amefunga jumla ya mabao 49 ambapo alifunga mabao 23 msimu wa 2018/19 na mabao 22 msimu wa 2019/20 na mabao manne msimu wa 2020/21 Meddie Kagere kuna hatihati akaukosa mchezo dhidi ya Yanga, Novemba 7 kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Kagere ana zali la kuwafunga Yanga ambapo kwenye mabao yake hayo 49 mawili aliwafunga Yanga, aliwafunga bao moja msimu wa 2018/19 Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikishinda bao 1-0 na kipa alikuwa ni Ramadhan Kabwili na aliwafunga 2019/20 kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 na kipa alikuwa ni Faroukh Shikhalo.

Kwa sasa dabi hiyo ya Kariakoo imebakiza siku 18 na Kagere yupo chini ya uangalizi akitibu majeraha yake aliyoyapata Oktoba 4 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma wakati Simba ikishinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania na yeye alitupia mabao mawili.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kikosi cha Simba kipo vizuri huku kikiwa na wachezaji wachache majeruhi waliopo chini ya uangalizi maalumu.
“Gerson Fraga anaedelea vizuri na John Bocco ameanza mazoezi mepesi. Pia Meddie Kagere ambaye kwa ukweli yeye atakuwa nje kwa muda wa wiki tatu kwa mujibu wa jopo la madaktari mpaka pale hali yake itakapotengemaa atarejea uwanjani.
“Matarajio yetu ni kwamba Wanasimba wataendelea kuwaombea wachezaji wetu ambao ni majeruhi ili warejee kwenye afya zao,” alisema Manara.
Wiki tatu ambazo ni siku 21 zinamfanya Kagere kutokuwa na uhakika wa kuivaa Yanga, Novemba 7 kwa kuwa anaweza kuwa fiti Novemba 6 huku mechi dhidi ya Yanga ni Novemba 7 jambo ambalo linaleta ugumu kwake kuanza kwenye mechi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ondoka na Mkwanja Kwenye Tsh. 160,000,000
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu.


Issa
Kagere hata awepo tareh 7 aijalishi kichapo kitawahusu wana msimbaz tu
Hopemwaikuka
Mungu atamsaidia atapona
Gabriel
Kagera wako vzur sana 👍
Mariam mtandama
Vizur
Saupha mohamed
Kagera jembe
Rehema
Kagera uko vzr
Sabrina
Asapo kuwepo fresh tu kuvuja kwa pakacha
Povel
Get well soon. MAMBA mk14🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Flomena
Kwan mchezaji ni yeye tu
Amiri Kayera
Janja janja ya tu ya Simba hiyo
aisha
Simbaaaaa wakali
Dorophina
Pole yake kagere simba inapengo la mfungaji mzuri katikati ya uwanja
magdalena
dah itakuwa bonge la pengo kwa wana simba ila atakuwa sawa hivi karibuni
Angelina
Getwell soon
Zeiyana
Ukiangalia pale clabuni simba hawana mpango nae tena kagere kwanza umri ushaenda wamesajiri wachezaji wengi sana zamu yake hishaisha kagere hatasugua benchi sana
Caroline
Kwetu rahaaa tuu
Lydia Emmanuel Magoti
Atakama kwenye Game hiyo kagere Kama atokuwepo kichapo kitawausu tuuu wafanye wafanyavyo simba kiboko yao subilini majabu iyo siku taree 7
warda
Tuko poa Hata bila Kagere
Salma ngende
Hongera kwao
Shani
N pig kubwa tareh 7
Elika
Namkubali sana kagere
Khadija
Kagere jeshi
Tatu
Hata hvyo kikosi cha simba kipo vizuri kina masteka kibao walisajiliwa msimu huu
Fatuma kasomo
Kagere yupo gud
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
felister
kwetu vicheko tu
Sauda
Get well soon Kagere
Mwajumah
Kagere fundi
Ernest
Habari mbaya kwa wanamsimbazi kumkosa Kagere kwenye derby