Uhaba wa washambuliaji unaendelea kuwatafuna Man City msimu huu. Gabriel Jesus na Sergio Aguero wanaendelea kuuguza majeruhi na hivyo Pep anakosa silaha zake za mashambulizi.
Kutokana na hali hii, Pep alinukuliwa akijutia kutosajili mshambuliaji katika dirisha la usajili lililofungwa mapema mwezi huu.
Aliyewahi kuwa mchezaji wa Man City – Micah Richards, anadhani timu hiyo inapoteza nafasi ya kumsajili mchezaji wao wa zamani [Daniel Sturridge] na pengine wanapaswa kumsajili kuziba mwanya huo.
Richards amenukuliwa akisema, “Ingekuwa rahisi kwa Daniel kuachana na soka lakini bado anahamu ya kufanikiwa.
“Mwaka jana alikwenda Uturuki kwa ajili ya kupata muda mwingi wa kucheza soka licha ya taarifa kuzagaa kwamba anaumia mara kwa mara. Alifanya vizuri akiwa na Trabzonspor kabla ya kufungiwa kwa kuvunja sheria za michezo ya kubahatisha.
“Kama atakujacheza tena soka basi itakuwa ni nje ya nchi lakini bado ninaamini kunatimu kwenye EPL bado zinahitaji huduma yake. Man City ninawaweka katika kundi hili. Kukosekana kwa Aguero na Gabriel ni nafasi kwa Sturridge kuwapa matokeo hata kama hatocheza msimu mzima.
“Kwa sasa ni kama watu wamesahau kabisa ubora wa Sturridge lakini bado anamuda wa kuwaonesha watu kiwango chake.” aliyasema haya wakati akiwa na Sky Sports kama mchambuzi wa soka.
Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.



aisha
Ni jambo jema walilofanya kumchukua sturrigde maana yuko vizuri sana
Hopemwaikuka
Fanyen mpango arud hapo
Fatuma kasomo
Nijambo zuri
Dorophina
Wafanye tu mpango hata kwa gharama yoyote maana hali ya timu inapoelekea sio pazuri kukosa washambuliaji ni hatari kwenye timu
Sauda
Man City wamelamba dume
Fatina mfigi
Duuuh majanga hayo
Mwajumah
Ni jambo zuri
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri wachamkie dili hilo
Tatu
Man city watafute mbadala LA sivyo watafeli sana
Ester jackson
Habari njema hizi
Sylvester
Kweli tumeshamsahau mtu huyu ila sidhani kwa sasa kama atakuwa na kiwango cha kuchezea Mancity
Sabrina
Duuh hatari
Khadija
Safi san man city
Elika
Safi sana
warda
Pole yao
Ernest
Kwa soka la sasa lilivyokuwa la ushindani ndani ya EPL, Sturridge sio mtu sahihi wa kuwasaidia Mancity.
Mwanahamisi
Safi sana
Amani Maeda
Visa vya timu kupoteza mafanikio kwa kuuguliwa na wachezaji muhimu kumezigharimu timu nyingi sana Duniani.
Povel
Sturridge co chaguo la pepe ndani ya city
Saupha mohamed
Nomaa
Zahara Omary
Nomaaa snaa