Mchezaji wa mbio za langalanga wa timu ya Mercedes – Lewis Hamilton, ni kati ya wanamichezo wenye majina makubwa duniani. Akiwa analisaka taji la 7 la F1, kwake kazi anayoifanya nje ya uwanja ni muhimu zaidi kuliko kuweka rekodi ya mataji.
Hii imetokea baada ya Hamilton kunukuliwa akisema ” ninajivunia zaidi kazi niliyoifanya ya kusisitiza usawa mwaka huu kuliko matarajio ya kubeba taji la 7.”
“Ushindi wangu hautobadilisha maisha ya watu. Kujaribu kuboresha maisha ya watu duniani – usawa wa haki za binadamu, hicho ndio kitu cha muhimu zaidi kwangu.”

Hamilton anaweza kubeba taji la 7 kwenye mbio za Turkish Grand Prix siku ya Jumapili endapo dereva mwenzake wa Mercedes (Valtteri Bottas) atashindwa kupindua matokeo kwa kumzidi Lewis kwa zaidi ya pointi 7.
Endapo Lewis atafanikiwa kubeba taji la 7, atakuwa ameweka rekodi sawa na Michael Schumacher. Lewis tayari ameshampiku Schumacher kwenye rekodi ya kuwa na idadi ya ushindi kwenye mbio nyingi.
“Nitajivunia zaidi kuwa na rekodi sawa na gwiji kama Michael. Lakini pia ni funzo kubwa sio tu kwa watoto bali kwa watoto wenye ndoto kubwa kuliko wanavyojifikiria na usikubali mtu akuambie hauwezi kuifikia ndoto yako.” Alisema Lewis Hamilton
Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!



Sabrina
Lewis hamilton mtu makini sana
Latifa juma mohamed
Hakika Hamilton ni mtu Makin Sana.
zeiyana
Hamilton hanatakiwa hapambane kupitiliza kwa maana mtu aliyeshindana nae ni gwiji wa mchezo huo
Sauda
Hamilton jembe
Carolyn
Hamilton yupo vizuri
magdalena
kama kazi anayoifanya ni nzuri zaidi bac aachane tu na ayo mashindano
Tatu
Hamilton yupo vizuri
Povel
Nice update
Ester jackson
Good news
David Pere
Endapo Lewis atafanikiwa kubeba taji la 7, atakuwa ameweka rekodi sawa na Michael Schumacher. Lewis tayari ameshampiku Schumacher kwenye rekodi ya kuwa na idadi ya ushindi kwenye mbio nyingi.
Mwajumah
Hamilton yupo vizuri sana