Clatous Chama, nyota wa Klabu ya Simba ameweka bayana mpango wake wa sasa ni kuitumikia timu hiyo na hana mpango wa kuibukia ndani ya Yanga.
Hivi karibuni habari zimekuwa zikieleza kuwa Yanga ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya nyota huyo raia wa Zambia ambaye ana tuzo ya mchezaji bora kwa msimu wa 2019/20 baada ya kutoa jumla ya pasi 10 na kufunga mabao mawili kati ya 78 yalifungwa na Simba.
Kwa sasa Chama mwenye pasi tano na mabao mawili kati ya 22 yaliyofungwa na Simba yupo zake nchini Zambia na timu ya Taifa ambayo jana Novemba 12 ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Botswana kwenye mchezo wa kufuzu Afcon.

Chama amesema:”Mimi ni mchezaji wa Simba kwa sasa sina mpango wa kwenda Yanga mjomba, bado nitakuwa ndani ya Simba ikitokea kutakuwa na mabadiliko yoyote kila kitu kitakuwa wazi,” .
Desemba 15 dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa Bongo ambapo jina ambalo limekuwa gumzo kwa sasa ni nyota huyo ambaye wengi hupenda kumuita mwamba wa Lusaka.
Habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa tayari wamemuongezea mkataba wa miaka miwili utakaomfanya abaki ndani ya timu hiyo yenye ngome yake Msimbazi.
Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!



Issa
Chama anawez kujiunga na wababe wa jangwan itakua poa
Hopemwaikuka
Atakavyo yy ndo hvyo hvyo
Sabrina
Chaka abaki tu simba
Fatuma kasomo
Baki tu chama
zeiyana
wachezaji siku zote wanaangalia maslai tu sio watu wakuwasikiliza sana chama mwili wake huoi simba moyo wake hupo yanga
Sauda
Yanga panamfaa sana
Fatina mfingi
Duuh nilitak kushangaa cham aende yang!!
Carolyn
Sisi Yanga tupo full.hatutaki wageni
Adelta
Abaki tu simba
magdalena
chama abaki tu simba yanga ataenda kufa njaa
Angelina
Bora abaki simba
Rahma
Abali tu simba
Lydia Emmanuel Magoti
Chama kubaki simba ni yeye mwenyewe mwenye mamuzi abaki au asibaki ila chama kutoka simba sio laisi yeye ndio amezilisha kuwa Mimi Bado nipo msimbazi mengine hayo maneno yawatu tumeyazoea
Antony Luseno
Kwa kauli yake apo ndo kakata mzizi wa fitina maana maneno yalikuwa ni mengi mno
Tatu
Yanga awana uwezo wa kumchukua chama
Povel
Bongo wamekuwah hawaelewek wanawez kubadili badilika muda wowote
aisha
Clatious cham mwamba wa lusaka anaweza kaz yake
Ester jackson
Tunaomba liwe kweli karibu sana chamani
David Pere
Bongo wamekuwah hawaelewek wanawez kubadili badilika muda wowote
Saupha mohamed
Abaki tu simbaa
Mwajumah
Chama na simba dam dam