Miaka ya 1990s John CruyfF’ aliabudu sana mfumo wa tiki taka na umiliki wa mpira kwa vijana wa La Masia pale barcelona, na ndipo soka likalipa fadhila kwa kumtunuku dunia ya kulia beki wake wa kulia ALBERT FERRER, akawa mtu na nusu.
Ferrer aliyaishi maajabu yake ya mguu wa kulia , alimwaga cross zilizompa magoli Ronald koeman na mwenzake Angel Nadal , muda huo hata Dani alves hakudhani kama ipo siku angevaa uzi wa barca kwani Dani alves hakufanya hata robo ya alichokifanya ferrer kwenye dunia ya kulia ya fc barca.
Miaka ya 2015 jina la Juma Abdul Mnyamani lilitawala sana masikioni mwa wengi, binafsi nilikufananisha na Henry mcKop beki wa Zimbabwe kongwe iliyocheza World Cup.
Wengi wakakushindanisha na Shomari Kapombe, Juma uliyamwaga maji kwa Donald Ngoma, Hamisi Tambwe na Simon Msuva, na kazi ya kufunga ikawa rahisi sana, tangu hapo moyo wangu ukazama kwako.
Nikaanza kustaajabu nilipomuona Paul Godfrey boxer akikuweka benchi hadi timu ya taifa, hapa ndipo dhambi ya usaliti ilipoanzia juma ,licha ya majeruhi ya muda mrefu ya kapombe, Juma bado haukutuita, nafasi bado ipo Juma, tufikirie na sisi, bado tunaihitaji huduma yako pale kwa Mkapa.
Kila nikitazama ile Yanga ya kampa kampa tena, huku Msuva pale Ngoma, katikati Kamussoko mbele yake Tambwe, kushoto Oscar Joshua, kulia nilikuwa nakona wewe, zile krosi zako zikanipeleka kijijini Novo Hamburgo nchini Brazil, mahala alipozaliwa beki wa kulia Maicon Douglas sessinado. Sikuchoka kukutazama.
Moyo wangu umejaa makelele ya lawama za wapenda soka, ningefurahi kumuona Kibwana Shomari anapata uzoefu kwako, kama anavyoupata Duchu kwa kapombe pale simba. Mitaa imekumiss Juma, unarudi lini?
Kuna vitu Ligi yetu inakosa kutoka kwako. Nimewaza zile cross zako angezikuta Michael Sarpong, zile V- pass zako zingemkuta Yacoba, na zile pass za Carlinho zingekufikia wewe, daaaaah, Jumaa, Ipunguze hii dhulma, tumeimiss ile ladha ya chocolate ya miguu yako.
Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!



Povel
Juma Abdul ni mmoja ya wachezaj wa beki ya kulia wanaoitendeah haki namba hyo natuamain hatafany vzr Zaid na kuvuka mipaka ya nje kwa uwezo anamkubwa wa kusaka kabumbu kila la kheri juma Abdul Mnyamani
Issa
Ni makini sana kwa timu kama hii
Issa
Anajituma sana ni mchezaji wa viwango vya juu
Hopemwaikuka
Dah ! Hii story imeishaje sasa
Sabrina
Daah hatari sana
Fatuma kasomo
Asante kwa taarifa meridianbet
zeiyana
labda kuna vitu tu vimeingiliana juu yake lakini bado juma abdul hajashuka viwango vyake kila la kheri mpambanaji
Sauda
Anajitahidi sana
Fatina mfigi
Ni mchezaji Makin sana
Carolyn
Asante kwa taarifa
Adelta
Anajituma Sana na kujituma akiwa uwanjani
magdalena
juma abdul katika kuucheza mpira anajua sana wampange tu vizuri atarudi
Angelina
Good update
Rahma
Nice
Lydia Emmanuel Magoti
Kijana yupo makini Sana anajituma sana
Dorophina
Habari njema sana
Tatu
Ni mchezaji mwenye kiwango anajituma sana
aisha
Beki makin sana moja ya mabek bora ligi ya tanzania
Ester jackson
Asante kwa taarifa
David Pere
Juma Abdul ni mmoja ya wachezaj wa beki ya kulia wanaoitendeah haki namba hyo natuamain hatafany vzr Zaid na kuvuka mipaka ya nje kwa uwezo anamkubwa wa kusaka kabumbu kila la kheri juma Abdul Mnyamani
Saupha mohamed
Juma yupo vizuri sana
Mwajumah
Ni makini sana kwa team kama hii