ATP Finals 2020: Nadal na Thiem Hawashikiki!

Kunako mashindano ya mchezo wa tenesi, ATP Finals 2020 imeendelea tena wikiendi hii. Rafael Nadal, Dominic Thiem na Novak Djokovic wakifurahia nyakati zao tofauti tofauti.

Rafael Nadal ameendelea kuwa bora katika juhudi zake za kuendelea kujikusanyia mataji. Hii ni baada ya kumfunga Andrey Rublev ambaye alikuwa anashiriki mashindano ya ATP Finals 2020 kwa mara ya kwanza.

Ushindi wa seti 6-3 6-4 ulimtosha Nadal kumchakaza Rublev. Kumuondoa Rublev ambaye yupo kwenye kiwango kizuri kwa sasa akiwa ni mchezaji pekee aliyeshinda michezo mingi na kubeba mataji mengi zaidi kuliko wachezaji wengine wanaoshiriki mashindano ya ATP mwaka huu, ni mwanzo mzuri kwa Nadal.

 

Rafael Nadal baada ya kumchakaza Andrey Rublev

“Nimefurahishwa na ushindi huu kwa sababu unabadilisha muelekeo wa mashindano haya kwa kiasi fulani. Ninajua nina mchezo mgumu dhidi ya Dominic, lakini kushinda mchezo huu kwa seti 2 za mwanzo kunaongeza uwezo wangu wa kujiamini.” Alisema Nadal.

Rafael Nadal anamachungu ya kukosa ubingwa wa ATP katika fainali mbili alizopoteza mwaka 2010 na 2013.

Ratiba ya muendelezo wa michezo ya ATP Finals 2020. (Chanzo – BBC)

Dominic Thiem alipata nafasi ya kulipiza kisasi kwa Stefanos Tsitsipas ambaye alimfunga kwenye fainali za ATP mwaka jana.

Bingwa wa US Open 2020 -Dominic Thiem alishinda kwa seti 7-6 (7-5) 4-6 6-3 katika mchezo uliochezwa kwenye ukumbi wa O2 Arena bila ya uwepo wa mashabiki.

“Kama ukianza kwa spidi ndogo huwezi kushinda. Miaka 4 iliyopita niliona umuhimu wa kuanza kwa kasi kubwa kwenye mchezo na ninafurahi nimefanya hivyo.” Alisema Thiem.

Kwingineko katika mashindano ya ATP Finals 2020: Djokovic abeba taji la mchezaji namba 1 duniani.
Novak Djokovic akabidhiwa taji la kumaliza mwaka akiwa mchezaji namba 1 duniani.

Kabla ya michezo ya ufunguzi ya ATP, Novak Djokovic alikabidhiwa taji la mchezaji aliyemaliza katika nafasi ya namba 1 duniani kwenye ATP Tour 2020.

Hii ni mara ya 6 kwa Djokovic kumaliza kama mchezaji namba 1 duniani, Novak anakuwa na rekodi sawa na mchezaji nguli wa tenesi – Pete Sampras.

“Ninajuvunia hili. Nimezidiwa na hisia za furaha ndani mwangu.” Alisema Djokovic baada ya kuwa na rekodi sawa na mchezaji anayempenda tangu akiwa mtoto.

Ushindi huu mkubwa kwa Djokovic umetokana na kushinda taji la 17 la Grand Slams mapema mwezi Januari katika mashindano ya Australian Open.

Anashiriki mashindano ya ATP Finals 2020 akiwa amepoteza michezo 3 pekee kati ya 42 aliyocheza mpaka sasa.


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

20 Komentara

    mambo yanzidi kupamba moto

    Jibu

    Nadal na Thiem naona wanazidi tunogesha tu mamb ya ATP finals 2020

    Jibu

    Hongera nyingi kwao

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Mambo ni moto

    Jibu

    Good

    Jibu

    Mambo yanazidi kunoga👏👏

    Jibu

    Mechi kalii

    Jibu

    Mambo ni fire

    Jibu

    Mambo yanazid kuwa mazuri

    Jibu

    Mambo yanazidi kuwa mazuri kwao

    Jibu

    Nadal hazini kutusua miamba ukichilia mbali na serena wakati wake sasa

    Jibu

    Hongera sana Nadal.unakuja vizuri sana.keep it up.

    Jibu

    Kwa raha zao

    Jibu

    Atp mambo ni moto

    Jibu

    Big up kwao

    Jibu

    Hao viumbe hatari ukiwakuta uwanjani

    Jibu

    Hongera yao

    Jibu

    Hongera yao

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.