Australian Open Katika Hali ya Sintofahamu.

Ratiba za mashindano kwenye michezo mbalimbali duniani zimeathiriwa na mlipuko wa COVID19. Upande wa tenesi, Mashindano ya Australian Open bado haijafahamika yataanza lini kutimua vumbi.

Australian Open hufanyika katika jiji la Melbourne nchini Australia na hofu imeanza kutanda kama mashindano haya yatafanyika mwezi Januari 2021 kulingana na ratiba ilivyokuwa imepangwa au itabadilika?

Taharuki hii inatokana na taratibu za kukaa karantini zilizowekwa na mamlaka za serikali ya Victoria ambapo imeripotiwa mamlaka hizitoruhusu wachezaji kuingia sehemu hiyo kuanzia katikati mwa mwezi Disemba, 2020.

Novak Djokovic Alibeba Taji lake la 8 la Australian Open mwezi Januari, 2020

Shirikisho la mchezo wa tenesi nchini humo – Tennis Australia lilitegemea kuwepo kwa uwezekano wa wachezaji kuanza kujiandaa ndani ya siku 14 za kukaa karantini kabla ya kuanza mchakato wa wiki 2 kuelekea kuanza kwa mashindano hayo.

Japokuwa taarifa zimeripoti kuwa, mpaka sasa serikali haionekani ikibadilisha msimamo wake licha ya kwamba kiongozi wa Victoria – Daniel Andrews alisema serikali bado ipo kwenye mazungumzo na Tennis Australia katika kuangalia utaratibu wa kukaa karantini.

“Tunaamini tutamalizana na Australian Open. Kuhusu wachezaji kuwepo hapa mwezi Disemba, hilo ni suala jingine.

“Sidhani kama hii inamaanisha hakutokuwa na Australian Open” alisema Andrews.

Pamoja na taarifa hizi, bado kuna uwezekano wachezaji wakaruhusiwa kuingia nchini humo mwishoni mwa mwezi Disemba. Hii itawapatia muda wa kujiandaa zaidi kabla ya michezo ya kufuzu kuanza kuchezwa Januari 12, 2021 kama ilivyopangwa.

Bado kuna namna kadhaa ambazo mashindano haya yanaweza kufanyika. Mashindano yanaweza kufanyika wakati wachezaji wapo karantini kama ilivyofanyika jijini New York kuelekea mashindano ya US Open.

Pia, Mashindano ya Australian Open yanaweza kurudishwa nyuma kwa wiki 1 au 2 ili kuwezesha michezo ya ufunguzi kuanza kama ilivyopangwa. Sambamba na hili, idadi ya timu shiriki inaweza kupunguzwa ili kupunguza idadi ya watu watakaoingia Australia kwenye mashindano haya.

Bado ni suala la muda na maridhiano baina ya wahusika wa mchakato huu ambapo Mashindano ya Australian Open ni kati ya mashindano makubwa kwenye ulimwengu wa tenesi.


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

29 Komentara

    corona inaharibu kila kitu, ratiba nyingi zinavunjika mno, mara zinasogezwa mbele ama vile.

    Jibu

    Corona bado ni janga kubwa

    Jibu

    Upande wangu me naona wanachofikiria kuwaweka wachezaji karantini n jambo zur sana ili kuweza kupata uwakika wa afya ya wachezaji maana michuano ya Australia open n wa ushindani mkubwa sana

    Jibu

    Coronavirus imeharibu ratiba mbali mbali katika ulimwengu wa soka

    Jibu

    Corona bado nitishio sana inabidi wafanye mbin mbadal ili wajue wataipuka vipi

    Jibu

    Corona bado inatikisa sana bado ni janga kubwa

    Jibu

    corona imepangua kila mipango mbalimbali iliyokuwa imepangwa

    Jibu

    Mungu tunaomba utuondolee corona

    Jibu

    Mh!!!!corona

    Jibu

    Kama vigezo na masharti vinazingatiwa kuna huwezekano mkubwa wa kulitokemeza hili gonjwa la hatari

    Jibu

    Hivi hili gonjwa ni lini litaisha ama tusilisikie kabisa

    Jibu

    Corona bado inaendelea kutuharibia burudani

    Jibu

    Hili janga sasa lishakua too much

    Jibu

    Corona tishio

    Jibu

    Wanacho kifanya kuwaweka karantini ni sawa mana inawapa kuwaangalia zaidi jinsi ya kuwakinga na corona ingawa pia inawaadhiri wanamichezo katika ubora wao Wa kimichezo hivyo wanatakiwa kama wanataka kufungua itabidi watagute mbinu zaidi ya kuwakinga wachezaji Wao

    Jibu

    Corona sio poa

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Hili janga litaisha lini? Dah

    Jibu

    Corona bado ni janga kubwa

    Jibu

    Sidhani kama mwafaka hautapatikana japo itachelewa

    Jibu

    Corona ni janga la dunia nzima

    Jibu

    Covid 19 bado janga la dunia

    Jibu

    Corona Sio poa kabisa

    Jibu

    Daah corona ingetuacha kidogo basi tufanye yetu

    Jibu

    duh corona sio poa kabisaaa

    Jibu

    Duu sio poa Corona imekuja kuludisha Mambo nyuma Sana michezo kuwailishwa

    Jibu

    Corona sio poa

    Jibu

    Asnt kwa taarif meridianbet

    Jibu

    Ao michuano migumu sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.