Luka Modric Kustaafia Madrid, Itawezekana?

Ulimwengu wa soka na mashabiki wa Real Madrid kwa upekee wao, wanautambua uwezo wa Luka Modric katika safu ya kiungo.

Mkataba wa Luka Modric unamalizika mwishoni mwa msimu huu na hakuna dalili kama anaweza kuongezewa mkataba mpya mpaka sasa.

Licha ya kutokuwa na dalili za mkataba mpya, Modric amefunguka kuwa anataka kuendelea kuwepo Madrid na ameenda mbali zaidi kwa kuongeza kuwa atakuwa mwenye furaha zaidi kama atapata nafasi ya kustaafu maisha ya soka akiwa Santiago Bernabeu.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter Milan leo usiku, Luka Modric amesema ” Nimesema hili (kwamba ninataka kubaki Real Madrid) mara nyingi lakini tusubiri tuone nini kitakachotokea. Kila mara ninatoa jibu lilelile, ninajisikia vizuri na ninataka kuendelea kuwepo Madrid.

Luka Modric

“Ninahisi ninaweza kuisaidia timu, kama utaniuliza ni nini ninahitaji, ninahitaji kubaki. Ninataka kumaliza maisha ya soka nikiwa hapa lakini hilo litategemea mambo mengi. Hakuna mtu atakuwa mwenye furaha kunizidi mimi kama nitastaafia hapa.

“Ninajisikia vizuri. Michezo ambayo sikucheza ni kutokana na maamuzi ya kocha na ninapocheza, ninajaribu kufanya vizuri.

“Wanaongelea sana hali yangu lakini tusubiri tuone ni nini kitatokea mbeleni.”

Je, Real Madrid watachukua uamuzi wa kumbakiza Luka Modric klabuni hapo au wataamua kuachana naye mkataba wake utakapo malizika? Madrid wameanza vibaya Ligi ya Mabingwa msimu huu wakiwa wameshinda mchezo 1 kati ya 3. Ushindi dhidi ya Inter leo usiku utawapa matumaini ya kuendelea kusalia kwenye Mashindano ya msimu huu.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

27 Komentara

    Inawezekana kwa sababu ni mchezaji mzuri wa Real madrid

    Jibu

    kaona madrid ndo panamfaa kustaafia

    Jibu

    Kama anaona panamfaa kustaafu akiwa apo ni vizuri zaidi kwan uamuzi ni wake yeye

    Jibu

    Modrick Madrid ungeendelea kukaa apo kwa kua.ndio timu yako pendwa

    Jibu

    Ndio patamfaa

    Jibu

    Inawezekana kabisa.

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Uwamuzi ni wake kama patamfaa

    Jibu

    Safii

    Jibu

    Maamuzi ni yakwake kama panamfaa hau laah!

    Jibu

    Sio mbaya ukibak hapo hapo

    Jibu

    Katika dunia hakuna kinachoshindikana

    Jibu

    Kila kitu kinawezekana

    Jibu

    Hapo ni maamuzi yake kuendeleah kucheza ndani ya madrid mpaka hatakapo fikiah final kucheza soka

    Jibu

    Panamfaa sana tyuu

    Jibu

    Modric ameona madrid ndio sehemu sahihi kwake kuitumikia mpaka atakapofikia hatua ya kustaafu

    Jibu

    Kiwango Modric kimeshuka na Madrid inatakiwa kusajiri wachezaji wenye viwango kuendelea kubaki ktk ubora na Kocha anamuona hana msaada tena ndio maana anamuweka bench

    Jibu

    Modric kustaafu madrid inawezekan ila kwa mchezaj kama huyu ambae historia inambeba atahitaj kuondokaa kuweka rekod timu zingin

    Jibu

    maamuzi yake kuendelea kucheza ndani ya madrid

    Jibu

    Asante kwa makala

    Jibu

    Gud

    Jibu

    Hakuna kinachoshindikan

    Jibu

    Panamfaa sana tu

    Jibu

    Modric akaona Pana mfaa apo ndomana anataka kustarfu apo

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Wamuongezee tu jamani

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.