Nyota wa Lazio Mohamed Fares ametoa mchango wa €2,500 kumsaidia mfikisha mizigo kutoa Napoli ambaye aliibiwa pikipiki yake ndogo aliyokuwa anaitumia kwa shughuli zake.
Gianni Lanciano, mwenye miaka 52, anafanya kazi kama mtu anayefikisha mizigo baada ya kupoteza ajira yake ya awali katika bucha fulani miaka mitano iliyopita.
Katika kipindi cha mwaka mpya, bwana huyu alivamiwa na wanaume watano ambao walitumia nguvu kumpora pikipiki yake.

Mamlaka za Italia kuweka wazi kuwa tayari wahusika wameshapatikana na kuwekwa kizuizini baada ya picha ya video iliyorekodiwa na mmoja wa wakazi wa tukio lilipotokea kurekodi na kusambaza video ya mkasa huo ambayo iliwafikia maelfu ya watu na kuzua hisia tofauti huko Italia.
Mchakato wa kumtafutia pesa muhanga wa tukio hili ulifanyika na kuwekwa katika mtandao wa GoFoundMe. Fares ni mmoja ya waliochangia ambapo alichangia €2500. Mpango huu ulikuwa na lengo la kufikisha kiasi cha €5000 lakini ndani ya masaa machache ilifika €10,000.
Mashabiki wa Napoli wamekuwa wakimpongeza Fares kupitia mitandao yao kwa wema wake kupitia tukio hili.
Ndio, kwetu Mteja ni mfalme. Jiunge sasa na familia ya Meridianbet bila malipo yeyote na sisi tutakuzawadia bonasi ya shilingi 3,500 kama sehemu ya kukukaribisha kwenye familia hii BURE!!!. Unasubiri nini??



Magdalena
Umoja ndo jambo zuri ni kuonesha upendo
Sania
Hongera kwake Farres,kutoa ni moyo
Shakila mrope
Habari njema
Angelina
Ameonesha upendo sana
Hopemwaikuka
Fares endelea na moyo huo huo
Chiku
Mungu atamuongezea alipo toa
Dorophina
Pongezi kwake fares kwa kitendo alichokifanya
Janeflora malisa
Safi
Caroline
Safi sanaaa
Ernest Kimeru
Pongezi kwa Fares
Sarah
Safi sana
Adelta
Pongezi kwa fares
Lydia Emmanuel Magoti
Pongezi zake
Issa
Saf kwake
Khadija
Kweli kutoa ni moyo
warda
jAMANI KAFANYA VIZURI SANA
Sabrina
Hongera sana