Mashabiki wa AC Milan wanatumaini kuwa nyota wao Zlatan Ibrahimovic atakuwa fiti kurejea dimbani kwenye gemu dhidi ya Juventus Jumatano.
Nyota huyu wa miaka 39, hajaweza kuingia dimbani tangia Novemba 22 alipopata jeraha kwenye mechi ambayo Milan walishinda Ugenini dhidi ya Napoli.
Milan wanakutana uso kwa uso dhidi ya Juventus Jumatano, Januari 6 na kwa mujibu wa chapisho la nyota huyu kwenye mitandao, amerejesha matumaini ya mashabiki juu ya kurejea kwake kwenye mechi dhidi ya Juventus.

Nyota huyu amechapisha video fupi akiwa mazoezini na kuandika maneno yanayoashiria mda si mrefu huenda akawa fiti dimbani. Katika video yake aliyochapisha aliambatanisha maneno ya “Tick tock tick tock.”
Nyota huyu wa zamani wa Inter na Manchester United leo amefanya mazoezi ya peke yake.Hata hivyo, baada ya ushindi wa jumapili kocha Stefano Pioli aliweka wazi kuwa hana uhakika nyota huyu atarejea lini na hawakua na mpango wa kumharakisha, lakini anaweza akawepo dimbani hivi karibuni.
Ndio, kwetu Mteja ni mfalme. Jiunge sasa na familia ya Meridianbet bila malipo yeyote na sisi tutakuzawadia bonasi ya shilingi 3,500 kama sehemu ya kukukaribisha kwenye familia hii BURE!!!. Unasubiri nini??



Rehema
Ni habari njema sana
Magdalena
Afadhali karejea maana tulikuwa tunamaubiria kwa hamu kubwa
Sania
Amefanya vizuri kurudi
Rahmal
Safi sana kuludi
Shakila mrope
Asante kwa taarifa
Angelina
Itakuwa vizuri kama atarejea
Hopemwaikuka
Mungu akupganie
Dorophina
Habari njema kwa mashabiki
Janeflora malisa
Safi
Caroline
Pole Sana movic
Mwanahamisi
Pole sana
Sarah
Akirudi itakuwa poa
Ernest Kimeru
Habari nzuri kwa Milan, Kesho Juventus wajipange
Adelta
Ni vizuri avyoamua kurudi
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri Sana
Issa
Cadaabra mwamba wa milan
Khadija
Vizur sana
warda
HATA MIE HUWA NAMKUBALI SANA
Sabrina
Yuko vizuri sana