Wakurugenzi wa AC Milan, Paulo Maldini na Frederic Massara wanaripotiwa kuwa wanafanya mazungumzo na wakala wa aliyekuwa nyota wa Juventus Mario Mandzukic.
Kwa mujibu wa chapisho la Calciomercato, mkurugenzi wa ufundi Maldini na mkurugenzi wa michezo Massara wanafanya mazungumzo juu ya uwezekano wa dili la nyota huyu wa Croatia.
Taarifa zinasema kuwa klabu ya Milan inataka kumpatia kocha Stefano Pioli uwanja mpana wa mbadala wa Zlatan Ibrahimovic, na mazungumzo tayari yanaashiria hatua kubwa ya mpango wao.

Taarifa nyepesi zinaainisha kuwa wakurugenzi hawa wanajaribu kukubaliana malipo na vipengele vya mkataba wa nyota huyu mwenye miaka 34 sasa.
Mandzukic aliachana na Juventus Januari mwaka jana, na akawa na mkataba wa miezi sita na Al-Duhail.
Nyota huyu tayari alishatumia miaka yake minne na nusu jijini Turin, akifanikiwa kufunga magoli 44 na kutoa assisti 17 kwenye mechi 162 alizocheza na Juventus.
MERIDIANBET INAKUPA NAFASI YA KUWA MILIONEA KWA KILA BAADA YA DAKIKA 5
Mchezo wa Keno unakupatia fursa ya kuibuka kidedea kupitia droo zinazochezwa kila baada ya dakika 5 tu!! Tunaposema Meridianbet ni nyumba ya mabingwa, tunamaanisha!!



Magdalena
Kila la kheri Milan
Issa
Kombineshen nzur na kadabra
David Pere
Mandzukic aliachana na Juventus Januari mwaka jana, na akawa na mkataba wa miezi sita na Al-Duhail.
Angelina
Nice update
Lydia Emmanuel Magoti
Kila la kheri
felister
kila la kheri
Hopemwaikuka
Vzur sana
Caroline
Sawaaa
Flomena
Nice
Sania
Kila la kheri
Ernest Kimeru
Itakuwa pouwa sana kama atatua Ac Milan
Dorophina
Mario ni bora haende milan
Khadija
Nice
Samira
Jambo zuri
Rahmal
Safi
warda
safi sana