Sven Alisepa Mwenyewe - Simba

Uongozi wa Klabu ya Simba umesema kuwa haukuwa na mpango wa kuachana na Sven Vandenbroeck ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Simba na alibwaga manyanga Januari 7.

Sven alisepa ndani ya Simba mazima ikiwa ni siku moja baada ya Januari 6 kuipeleka timu hiyo hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum umewapa tiketi Simba kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu ndani ya Klabu ya Simba, Crestius Magori amesema kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba,(Barbara Gonzalez) alipigiwa simu na watu kutoka sehemu aliyokuwa anakaa Sven na kuambiwa kuwa amebeba kila kitu mpaka viatu.

“Hatukuwa na mpango wa kuachana na Sven ila yeye mwenyewe aliamua kuondoka na CEO,(Barbara) alipigiwa simu na kuambiwa kuwa mbona kocha amebeba kila kitu kutoka kwa watu wa sehemu aliyokuwa anakaa.

“Ilikuwa ni asubuhi wakati huo timu ilikuwa inajiaandaa kwenda Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Kombe la Mapinduzi.

“CEO alimpigia simu Sven ambapo alisema kuwa bado yupo hana mpango wa kuondoka ila timu imeanza safari mchana ndipo anamwambia CEO kwamba kuna matatizo ya kifamilia anahitaji kuondoka.

“Hata ambapo aliambiwa kwamba kama ishu ni familia basi ilete hapa Tanzania kuna shule akasema kwamba ana ofa kibao ikiwa ni pamoja na Morocco ambapo ni karibu na Ublelgiji, sasa hapo hatukuwa na namna ikabidi tumuache aondoke,” .

Sven kwa sasa yupo ndani ya Klabu ya FAR Rabat ya Morroco akiwa ni kocha mkuu na Simba inanolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa.


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

10 Komentara

    FAR Rabat waliongeza mkwanja kwa Sven au kuna mengine

    Jibu

    Nimamuzi yake yeye

    Jibu

    Sven aliona aondoke tu kwa sababu kule kuna maslai zaidi

    Jibu

    Ni yy tu

    Jibu

    Sven naona alikuwa anatafuta maslai yalipo

    Jibu

    Kwani kambi kokote

    Jibu

    Sven alikuwa bado anatarii anatafuta penye mkwanja wa maana na ndo kilichomfanya asepe Simba baada ya kupapata penye unafuu wa mkwanja

    Jibu

    Mamuzi anayo mwenyewe

    Jibu

    Maisha popote

    Jibu

    Nitammic sana kishingo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.