Katika hali ambayo wengi hawakuitarajia, Juventus imeondolewa kwenye Mashindano ya Ligi ya Mabingwa ikiwa ni msimu wa 3 mfululizo haijafika hatua ya nusu fainali.
Juve walijikuta wakiangulia pua kwenye mikono ya Ajax kwenye hatua ya robo fainali (2018/19) kabla ya kuadhibiwa na Lyon (2019/2020) kisha msimu huu wakapoteza dhidi ya FC Porto.
Huu ni muendelezo wa matokeo mabaya ya Juve baada ya kukamilisha usajili wa Cristiano Ronaldo kwa ada ya pauni milioni 85. Kiuhalisia, usajili wa CR7 ulilenga zaidi kuisaidia Juve kutwaa ubingwa wa UEFA lakini hali imekuwa tofauti sana.
Itakumbukwa msimu uliopita, Juve walimfukuza kazi Kocha wao Maurizio Sarri baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye Mashindano ya UEFA licha ya kubeba taji la Serie A.

Baada ya kuondolewa kwenye mashindano hayo, kumeibuka taharuki kuhusu hatma ya CR7 na kocha Andre Pirlo kwenye kikosi cha Juventus. Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo – Fabio Paratici , ameamua kusafisha hali ya hewa kwa kusema kuwa, “bado kuna mwaka mmoja kwenye mkataba (mpaka Juni 2022).
“Kuongeza mkataba wa Cristiano Ronaldo sio kipaumbele kwa sasa, bado kuna mda wa kulizunguzia hilo.”
Juventus bado wanakibarua cha kutetea ubingwa wao wa Serie A msimu huu wakiwa wamezidiwa pointi 10 na vinara wa ligi hiyo, Inter Milan.
Ni Burudani Iliyokithiri na Mkwanja Nje Nje Katika Mchezo Halisi wa Chicago Gold.
Fanikisha malengo yako bila kuumiza kichwa, tengeneza mkwanja bila wasiwasi na kasino ya Meridianbet. Jiunge sasa Ufurahie Chicago Gold kasino.



warda
Kweli ni suala la mda tu mana wakifanya papara watapata tabu sana
Venerose
Juventus watajipanga upya
Lydia Emmanuel Magoti
Watakuwa sawa
Hopemwaikuka
Inapendeza
Caroline
Cr7 yupo vizuri
Neema juma
Ni kweli kabisaa na wanachokisema
Sarah
Watakuwa sawa
Issa
Asepe tu