Tetesi zinasema mshambuliaji wa Tottenham Jermain Defoe anaamini kuwa Harry Kane, 27, anahitajika kuondoka Spurs ikiwa anataka kushinda mataji.
Tetesi zinasema Barcelona inataka kuendeleza mkataba wa mashambuliaji wa Ufaransa, 23, Ousmane Dembele ambaye mkataba wake unakamilika 2022.
Tetesi zinasema Manchester United ilishindwa kumsajili Dembele msimu uliopita lakini bado imeonesha nia ya kumsaka mchezaji huyo na ina mawasiliano na wakala wake.

Juventus iko tayari kumtumia mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27, ambaye mkataba wake unakamilika Juni 2022, kama sehemu ya makubaliano ya mabadilishano kadhaa ikiwemo kiungo wa kati wa Manchester United Ufaransa Paul Pogba, 28.
Tetesi zinasema mlinda lango wa Ufaransa Hugo Lloris, 34, huenda akasalia Tottenham msimu huu licha ya makubaliano yake ya sasa kumalizika msimu wa mwaka 2022.
Manchester United imeanza mazungumzo na AC Milan kumjadili mlinzi wa klabu hiyo ya Italia anayetimiza miaka, 22, raia wa Ureno Diogo Dalot ambaye yuko huko kwa mkopo kubadilisha makubaliano yake kuwa ya kudumu.
Liverpool imeandaa pauni milioni 15 kujaribu kumsajili mlinda lango wa Uturuki Ugurcan Cakir kutoka Trabzonspor, huku RB Leipzig na Sevilla pia wakimnyatia mchezaji huyo, 24.
Aliyekuwa mlinzi wa Arsenal, Bacary Sagna anasema hatashangaa ikiwa beki wa kulia wa Uhispania Hector Bellerin, 26, ataondoka Gunners.
Serb Aleksandar Kolarov, 35, huenda akaondoka Inter Milan mwisho wa msimu akielekea Bologna moja ya vilabu vitano vyenye kumuhitaji mchezaji huyo aliyekuwa mlinzi wa Manchester City.

Kiungo wa Real Madrid na Ujerumani Toni Kroos, 31, yuko tayari kustaafu soka ya kimataifa baada kupata ushindi katika michuano ya Ulaya msimu huu.
Bale atakuwa mmoja wa wachezaji sita Real Madrid inawaruhusu kuondoka ili kupata fedha kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji wa Kifaransa anayekipiga Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22 na mshambuliaji Erling Braut Haaland wa Borussia Dortmund.
Chelsea inaungana na Manchester City kumnyatia Lukaku, ambaye amefunga mabao 59 baada kuchezea mechi 85 Inter Milan.
UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.
Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?



Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri
Adelta
Tetesi zinasomeka vizuri
warda
safi