Kitendo cha Cristiano Ronaldo Kususa baada ya kuona goli la Ureno limekataliwa hakikubaliki, hii ni kwa mujibu wa Fernando Meira, ambaye anasema mshambuliaji huyo anapaswa kuwa mfano bora kama nahodha.

Ronaldo alifikiri amewapa Ureno alama zote tatu wakati wa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Serbia Jumamosi baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Nuno Mendes na kupeleka wavuni.
Jitihada za mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 ni kweli zilivuka mstari licha ya Aleksandar Mitrovic kurudi kuokoa mpira, lakini mwamuzi aliruhusu mpira kuendelea baada ya kushauriana na wasaidizi wake, na kumpelekea mshindi wa Ballon d’Or mara tano kupata hasira kali.
Ronaldo alitupa kitambaa cha unahodha wake chini na kuondoka uwanjani baada ya kuona bao limekataliwa, na mechi hiyo ikamalizika kwa 2-2.
Meira anafikiria mchezaji mwenzake wa zamani alikuwa sahihi kuuliza uamuzi huo, lakini alihisi alikwenda mbali sana na kitendo chake kutokana na majukumu yake kama kiongozi wa timu ya kitaifa.
“Kitendo cha Cristiano ni cha asili, lakini halikubaliki kwa nahodha wa timu ya kitaifa,” mchezaji huyo wa zamani wa Ureno aliiambia Record.
“Hawezi kutupa kitambaa chini na kwenda kwenye vyumba vya kubadili nguo wakati mchezo unaendelea. Haikubaliki kwa mchezaji mwenye umuhimu wake.
“Ninaelewa kuchanganyikiwa kwake na ninakubaliana naye kwa sababu goli lake lilikuwa halali, lakini waamuzi wanapaswa kufanya maamuzi, bila VAR, na anapaswa kuonyesha mfano.
Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.



Caroline
Anasusaje kwa mfano
neema juma
Kaona bora asusee khaa
Adelta
Ronald ajafanya vizuri
warda
Jamani aliumia sana