Luka Modric amekubaliana na Real Madrid kusaini dili mpya ya mkataba rais Florentina Perez amesema.

Kiungo huyo wa Croatia mwenye umri wa miaka 35 ambaye alijiunga na Madrid akitokea Tottenham mwaka 2012 mkataba wake wa sasa unatarijia kuisha mwezi Juni.
Ripoti za mwezi Januari zilidai dili mpya kati ya Modric na Real Madrid tayari imeshakubalika lakini hakuna kitu chochote ambacho kilitangazwa.
Perez alithibitisha taarifa hizo siku ya Jumatano wakati wa majadiliano juu ya European Super League, wakati pia alitoa taarifa juu Sergio Ramos ambaye atakuwa nje mkataba mwisho wa msimu.
” Modric tayari amesaini au tulifikia makubaliano muda mrefu tu,” Perez alisema katika kipindi cha redio El Laguaro.
“Ramos hakupo katika hali kama hiyo, tumeongea mara nyingi lakini sijui, sitaki kumlaumu yeyote.”
Perez alikataa kuongelea hatima ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35.
“Nampenda unaweza kusema ni mwanangu, nitafanya kila ninachoweza kwaajili yake,” Perez alisema.
“Sitowaambia chochote kuhusu Sergio Ramos, tuna jaribu kumaliza msimu kisha tutaongea kinachofuata.”
Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.



Elika
Kijana yuko vizuri
Johnmary jo
Amefanya vizuri husain mkataba mpya na pia ni mchezaji mzuri#meridianbett#
Adelta
Luka Modric yuko vizuri
Venerose
Safi sana Luka
Issa
Kiungo bora sana
Theonestina
Duuuh
aisha
Kijana machachali huyu
dorophina
Kila lakheri modric
Khadija
Safi sana
Magdalena
Sa itakuwaje
Lydia Emmanuel Magoti
Duuh
warda
Huo ni usanii sasa