Guadiola Kufanya Maamuzi Magumu kwa Aguero

Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa anataka kumuona mshambuliaji wake Sergio Aguero anaonyesha kiwango cha juu uwanjani na anahitaji kumuona akicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kiwango cha nyota huyo ndani ya kikosi cha City kimezidi kuporomoka kwa sasa jambo ambalo limekuwa likimfanya akose kujiamini.

Pia kwa sasa imekuwa ikielezwa kuwa Guardiola hana uhusiano mzuri na Aguero jambo ambalo limekuwa likimfanya awe anamuweka benchi.

Guadiola and Aguelo

Aguero msimu utakapomeguka anasepa mazima kwa kuwa mkataba wake unakwisha na timu ilitoa taarifa rasmi kwamba hataongeza mkataba.

Guardiola amesema:”Nafikiri kwenye mchezo dhidi ya Newcastle alikuwa hayupo fiti lakini hata sasa bado hajawa fiti asilimia 100, nafikiri atakuwa tayari kwa michezo kadhaa.

“Bado kuna michezo kadhaa na ninadhani nitafanya maamuzi magumu katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Chelsea nafikiri anaweza kucheza,“.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

BASHIRI SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.