Ureno imepokea habari mbaya ya mchezaji wao Joao Cancelo siku tatu tu kabla ya mechi yao ya ufunguzi kwenye Mashindano ya Ulaya. Joao Cancelo amefamyiwa vipimo na kubainika na virusi vya corona na sasa atakosa mashindano, huku Diogo Dalot akikaribia kuingia kuchukua nafasi ya beki huyo wa kulia wa Manchester City.
Huu ni mwanzo mbaya kwa mashindano hayo kwa Ureno, ambao sasa hawana beki wao wa kulia tegemezi, ambaye amecheza vyema kwenye mechi za klabu yake msimu wote.
Cancelo alipimwa na kuwa na majibu yaliyoonesha kuwa na antigen na matokeo yake yalithibitishwa na jaribio la PCR lililofuata.
Wachezaji wengine wote kwenye kikosi walipimwa hawakuwa na maambukizi na shirikisho la mpira wa miguu la Ureno lilithibitisha tukio hilo na kwamba Dalot wa AC Milan atachukua nafasi kuziba pengo la Cancelo.
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.



Issa
Covid noma
magdalena
Pole yake