Kaizer Chiefs Yatinga Fainali CAFCL 2021

Baada ya kuingia kwenye hatua ya robo fainali, watu wengi waliibeza sana lakini ni rasmi sasa Kaizer Chiefs wametinga hatua ya fainali ya kombe la klabu bingwa Afrika baada ya kuingia katika michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Kaizer Chiefs ambao walikuwa wakicheza na Waydad Casablanca jana usiku katika mechi ya marudiano walifanikiwa kutoka sare ila goli moja walilopata katika mechi ya mkondo wa kwanza kule Morocco ikawabeba na sasa wapo fainali.

Mechi ya mkondo wapili iliyopigwa jana ilishuhudia Kaizer wakicheza kwa tahadhari sana huku wakishambulia kwa nafasi na mpaka dakika tisini zinakamilika, Kaizer 0, Waydad Casablanca 0.

Hivi sasa Kaizer Chiefs watakutana na mabingwa watetezi wa Kombe hilo Al Ahly ambao nao wametinga hatua ya fainali baada ya hapo jana kumpiga Esperance ya Tunisia 3-0, na kuwa magoli ya ujumla ya 4-0.

Mashabiki na wadau wengi wa soka Tanzania wanaamini kwamba nafasi aliyo the Amakhos kwa sasa ilitakiwa kuwa ya Simba endapo wangekuwa na bahati kidogo tu, lakini kiukweli ni kwamba Simba hawakujitoa sana katika mechi ya robo fainali ya mkondo wa kwanza.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.