Timu za Italy na Denmark zimekuwa za kwanza kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Euro 2020, baada ya mchezo mzuri na mkubwa walioonesha katika mchezo wa raundi ya 16 jana usiku.
Wales iliyokuwa chini ya Gareth Bale ilipata kipigo kikubwa sana cha 4-0 kutoka kwa Denmark, ambao walikuwa katika usiku mzuri sana na walicheza kwa kujiamini sana na kujihakikishia wanatinga robo fainali.

Mechi kati ya Italy na Austria ililazimika kwenda mpaka dakika 120 kutokana na timu hizo mbili kutoka sare dakika 90 bila timu yoyote kupata goli lolote licha ya kushambuliana kwa wakati na kucheza katika kiwango kikubwa sana.
Katika dakika 30 za nyongeza, Chiessa alikuwa wa kwanza kuandika goli la kwanza la Italy akipokea pasi murua kutoka kwa Leonardo Spinazzola na baadae katika dakika ya 105, Italy ikapata goli la pili kutoka kwa Matteo Pessina aliesaidiwa na Acerbi.
Mnamo dakika ya 114, Austria walipata goli moja liliwarudisha mchezoni kutoka kwa Sasa Kalajdzic ambaye alifanya Austria kuamka na kuanza kushambulia sana lango la Italy bila mafanikio yoyote.
Leo hii kutakuwa na mechi nyingine kali kabisa, Belgium watakutana na Portugal, hii itakuwa ni mechi ya kukata na shoka na si ya kukosa, Pita Meridianbet na uweke ubashiri wako sasa!


