Jorginho ni mmoja wa wagombea wa tuzo ya Ballon d’Or 2021 ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi kufuatia kuwa na msimu mzuri uliyopita akifanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa na Euro 2020.
Sasa kiungo huyo wa Chelsea anaamini kama akifanikiwa kushinda tuzo hiyo ataleta motisha kwa wachezaji wengine ambao sio wafungaji na kudhihirisha kwamba kigezo cha kushinda tuzo hiyo siyo magoli pekee.
Mchezaji huyo aliibuka mchezji bora wa kiume wa UEFA wa mwaka mnamo Agosti baada ya kuisadia Chelsea kushinda UCL na Italia EURO 2020.
Jorginho ambaye amefunga mabao nane kwenye mashindano yote msimu huu anachuana na Robert Lewandowski na Lionel Messi ambao ndiyo wapinzani wakuu kutwaa tuzo hiyo kubwa ulimwenguni.
“Sio swala langu kusema kama natakiwa kushinda Ballon d’Or lakini italeta motisha kwa wachezaji wengine kuonyesha kwamba magoli siyo kigezo pekee kinachozingatiwa,” alisema Jorginho.
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?