Mshambuliaji wa timu ya Manchester United Marcus Rashford na winga wa timu hiyo ambaye kwa sasa yuko kwenye kiwango kizuri Jadon Sancho wameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambacho kitacheza kwenye michezo dhidi ya Switzerland na Ivory Coast kwenye dimba la Wembley.
Marcus Rashford hajafanikiwa kuitwa kwenye kikosi cha Uingereza tokea kumalizika fainali ya euro ambayo alikuwa miongoni mwa wachezaji waliyokosa penati, huku siku za karibuni akiwa kwenye kiwango kibovu na kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya siku ya jumatano ilisambaa video ambayo ilimuonesha akiwatolea maneno machafu mashabiki.
Timu ya Uingereza imeshafuzu kwenye mashindano ya kombe la dunia nchini Qatar, na wanataka kuitumia hii michezo ya kirafiki kama maandalizi na kuweka umoja kwenye kikosi chao
Maguire na Shaw ni wachezaji pakee kwenye kikosi cha Manchester United waliyoitwa na kocha Gareth Southgate, kikosi kamili cha Uingereza kilichoitwa ni;
Magolikipa: Jordan Pickford (Everton), Nick Pope (Burnley), Aaron Ramsdale (Arsenal)
Walinzi: Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Conor Coady (Wolves), Marc Guehi (Crystal Palace), Reece James (Chelsea), Harry Maguire (Manchester United), Tyrone Mings (Aston Villa), Luke Shaw (Manchester United), John Stones (Manchester City), Ben White (Arsenal)
Viungo: Jude Bellingham (Borussia Dortmund), Conor Gallagher (Crystal Palace), Mason Mount (Chelsea), Jordan Henderson (Liverpool), Declan Rice (West Ham), James Ward-Prowse (Southampton)
Washanbuliaji: Tammy Abraham (AS Roma), Phil Foden (Manchester City), Jack Grealish (Manchester City), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Bukayo Saka (Arsenal), Emile Smith Rowe (Arsenal), Raheem Sterling (Manchester City)
SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI
Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.