Christian Eriksen ameitwa tena katika kikosi cha timu ya taifa ya Denmark kwa mara ya kwanza tangu alipota tatizo la moyo mwaka jana wakati wa mashindano ya Euro 2020.
Denmark wanajiandaa kwaajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Uholanzi na Serbia mwezi huu, na mchezo dhidi ya Serbia utapigwa tena katika uwanja ambao Eriksen alipata tatizo la moyo wakati wakicheza dhidi ya Finland.
“Ninatarajia Christian kuingia na kuwa sababu ya kuamua kwa timu yetu,” Hjulmand aliambia gazeti la Denmark Ekstra Bladet. “Sikutarajia angecheza hivi sasa, kiuhalisia nilidhani atakuwa tayari kufikia majira ya joto. Hata hivyo Christian yuko na kikosi kwa sababu yeye ndiye bora katika nafasi hiyo.”
Denmark tayari wamefuzu kwenda nchini Qatar kwaajili ya mashindano ya kombe la Dunia 2022 na Eriksen alisema ilikuwa ni malengo na ndoto kushiriki kwenye michuano.
SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI
Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.