Roberto Mancini ataendelea kuinioa timu ya taifa ya Italia licha ya timu yake kushindwa kufuzu mashindano ya kombe la Dunia kwa mara ya pili mfurulizo mara ya kwanza ilikuwa nchini Urusi na mwaka huu nchini Qatar.

Roberto Mancini aliongoza timu ya taifa ya Italia kuchukua ubingwa Ulaya miezi nane iliyopita, lakini amepoteza kwenye robo fainali ya kutafuta nafasi kushiriki michuano ya kome la Dunia nchini Qatar dhidi ya Macedonia.

Roberto Mancini
Roberto Mancini

Kocha Gian Piero Ventura alionyeshewa milango ya kutokea baada ya kishindwa kufuzu kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018, ambapo Ufaransa ndiye aliyekuwa bingwa wa michuano hiyo.

Ingawa chama cha soka nchini Italia kipindi hiki wameamua kubaki na Mancini ambaye alirudisha hamasa kwenye timu na kuingoza kuchukua ubingwa wa Euro 2020, kocha huyo mwenye miaka 57 bado anamkataba na shirikisho hilo ambao utaisha mwaka May 2026.

“Tunahitaji kuanza upya, nimezungumza na raisi wa shirikisho, tumekubaliana kwenye kila kitu ambacho tumezungumza na nini tuboreshe. Bado kijana na nilihitaji kushinda Euro na kombe la dunia, itabidi tusubiri kwa muda kidogo.

“Naipenda hii kazi na najua tukiungana na wachezaji tunaweza fanya kitu bora kingine, ukiachana na matokeo mabovu kila kitu kinaendea vizuri.” Mancini alisema


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa