Rio Ferdinand: Sioni Ronaldo Akiondoka Man Utd Msimu Huu

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Rio Ferdinand amesema kuwa haoni mchezaji mwenza wa zamani Cristiano Ronaldo kuondoka kwenye klabu hiyo kwenye majira ya kiangazi hata kama watashindwa kufuzu klabu bingwa barani ulaya.

Rio Ferdinand amecheza pamoja na Cristiano Ronaldo kwenye klabu ya Man Utd kuanzia mwaka 2003 hadi 2009, ambapo walikuwa chini ya kocha Sir Alex Ferguson huku wakifanikiwa kuchukua ubingwa wa ulaya, ubingwa wa Uingereza mara tatu, FA Cup mara moja na kombe la ligi mara mbili.

Rio Ferdinand
Rio Ferdinand

Ronaldo amejiunga na klabu ya Man Utd majira ya kiangazi mwaka 2021, lakini tokea amejiunga kumekuwa na tetesi za kuwa anaweza kuondoa ikiwa tu, timu hiyo itashindwa kufuzu kushiriki klabu bingwa barani Ulaya.

“Sioni kama ataondoka, nataka kuwa mkweli kwako, hata kama Man Utd wakishinda kuingia kwenye nne bora, alisema Rio Ferdinand.

“Nafikili Ronaldo anapaswa kushugulika na Man Utd kwa mwaka mwingine. Ndio anataka kushindana, anayo hiyo hamasa ya kutaka kushinda mataji, alishaozoea kufanya hivyo, amezoea kushinda tu.

“Lakini mara zote haiwezi kuwa hivyo, amekuwa na misimu mizuri karibia miaka yake yote. Ronaldo kutokushiriki michuano ya ulaya muziki kulia kwenye masikio yake kwenye usiku wa ulaya, sijui ni nini anafikili ikiwa atakuwa anasikili mziki mwingine ukichezwa.” Aliongezea Rio Ferdinand.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe