Klabu ya Brentford imempa dili ya mkataba mpaka mwisho wa msimu mchezaji Christian Eriksen ambaye alikuwa ni mchezaji wa Inter Milan siku ya Jumatatu ambapo ndiyo mwisho wa usajili wa Januari.
Mchezaji huyo wa miaka 29 anapasa kufaulu vipimo kujihakikishia yupo sawa kurejea kucheza tena baada ya kuwekewa kifaa kinachomsaidia kuratibu mapigo ya moyo baada ya kupata tatizo la shambulio la moyo wakati wa michuano ya Euro 2020.
Eriksen ameweka bayana kuhusu mkataba wa muda mfupi hadi mwisho wa msimu, lakini hatajiunga na kikosi cha Brentford wiki hii.
Siku chache zilizopita amepokea chanjo yake ya COVID-19 wakati akifanya mazoezi na Ajax huko Uholanzi, kwa hivyo anahitaji kutengwa kwa siku chache kabla ya kusafiri kwenda Uingereza.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Eriksen kucheza katika ligi ya Uingereza hapo nyuma aliwahi kucheza akiwa na Tottenham kwa miaka sita kabla ya kutimkia Inter Mwezi Januari 2020.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.