Dakika takribani 87 za jasho na damu zilikatika bila kuelewa hatima ya mechi, Simba walishambulia Azam na wao wakajibu kwa wakati wao. Ila ilihitajika akili ya wakili msomi, BM3 kuleta mabadiliko na kumpa mnyama ushindi mnono wa 1-0 dakika za jioni.
katika mechi iliyojaa vita na akili pamoja na nguvu nyingi eneo la kati, Viungo wa wa Msimbazi walipata tabu sana kutoka kwa Mudathir Yahya ambaye alisaidiwa vyema sana na Brayson Rafael.
Kuingia kwa Benard Morisson katika kipindi cha pili kuliifanya Simba kuwa imara sana katika eneo la pembeni ambapo kwa pande zote mbili ambapo Morisson alikuwa akibadili upande kadri apendavyo.
Bruce Kangwa alimchezea rafu Benard Morisson ambaye alianzisha mchezo wa haraka na akampasia Luis Miqsone ambaaye hakufanya hajizi na kupachika goli moja kali na kuipeleka vijana wa Gomes hatua ya fainali kule Kigoma.
Sasa ni rasmi Simba itakutana na Yanga tarehe 25 mwezi wa saba baada ya kukutana mapema mwezi wa Saba tareh 3 kucheza mechi ya kiporo iliyoahirishwa mnamo tarehe 8 mwezi wa tano kutokana na mabadiliko ya ratiba.


